Elections 2010 Ubunge viti maalumu, hesabu zipoje?

Elections 2010 Ubunge viti maalumu, hesabu zipoje?

MpigaFilimbi

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2008
Posts
1,169
Reaction score
187
Wakuu,
Nimekuwa nikisikia harakati zinazoendelea huko CCM kuhusu kuwania viti maalumu wanawake, walemavu, vijana, wafanyakazi na zingine. Inavyoonyesha karibu kila mkoa wanatoa washindi wawili ambao wanatangazwa kuwa wameshinda viti maalumu. Sielewi hizi hesabu zinaendaje, hasa ukizingatia kuwa idadi ya mikoa ya Tanzania na idara zote zilizopo CCM, hainiingia akilini kuwa tunahitaji kuwa na wabunge wote hao kwa fedha za walipa kodi ambao kimsingi hakuna wanachokifanya zaidi ya kuongeza uwingi au kura za CCM.
Nilichokuwa najua ni kuwa viti maalumu vinatolewa kutokana na asilimia ya wabunge ambao chama husika inapata katika uchaguzi mkuu, inakuwaje hao wanatangazwa washindi wakati hawajui kwa yakini hicho chama chao kitapata asilimia ngapi ya wabunge kwenye uchaguzi ujao? Inawezekana ninakosa facts, mwenye ufafanuzi tafadhali....
 
mwisho wa siku uamuzi wa mwisho utatokana na idadi ya wabunge wa kuchaguliwa waliopatikana na idadi ya kura za urais za chama husika. so hayo ni maendekezo ya awali tu
 
Back
Top Bottom