Mnyika wala huwezi kumlinganisha na Nape. Mnyika ana uwezo zaidi wa uongozi na ana mtaji tayari katika jimbo. Nape nina wasiwasi kama atapita ndani ya mchuzo wa chama chake. Hata akipita atakuwa majeruhi tayari wakati Mnyika atakuwa anasubiri majeruhi gani wa kudili nae. Nape bora atafute jimbo lingine la Dar. Ubungo ni ya CHADEMA, Ubungo ni ya Mnyika!
tatizo la Nape tayari anajiona kamaliza safari kabisa....pia personal issues zitamponza, katika umri alionao si busara aendelee kukaa kwa baba mkwe wake pale Jesus Village-Changanyikeni, itashusha imani kwa wapiga kura...pia hana ukaribu na vijana wengi waliopanga pale kwa baba mkwe wake, Brigadia Hemed, wanamlaumu sana kwa kujifanya hana time hata na salamu tu..na mwisho kabisa,ukiwaweka Nape na Mnyika kwenye mjadala, Nape ataachwa mbali sana...but tusubiri tuone coz hata Shamsa nae yumo..
Please wanaJF naomba kujua academic profile ya Nape.
KWA MUJIBU WA MAHOJIANO YAKE NAPE NA GAZETI MOJA NCHINI HII NDIO ACADEMIC PROFILE YAKE, TUWEKE NA YA MNYIKA TUPIME!Please wanaJF naomba kujua academic profile ya Nape.
KWA MUJIBU WA MAHOJIANO YAKE NAPE NA GAZETI MOJA NCHINI HII NDIO ACADEMIC PROFILE YAKE, TUWEKE NA YA MNYIKA TUPIME!
...Shule ya msingi
...Sekondari
....Sekondari ya juu..form six
....Stashada ya Sayansi Jamii-Kivukoni
....Stashahada ya Diplomasia,Uhusiano wa kimataifa na stretegic stidies
...Shahada ya Saikolojia,Lugha na Habari
....Stashahada ya Ushaiuri nasaha
....Stashada ya matumizi ya computer...diploma in computer application
.... Certificates kadhaa katika fasihi ya kingereza na kifaransa
... Na sasa anasoma shahada ya pili ya Public Administration
Kuweka madaraja aliyosoma bila kuonesha chuo alichosoma na miaka yake ni kuonesha wazi kua you are hiding some facts somewhere. Anyway usiendelee kuongea zaidi acha hivyo hivyo tutaelewa tu. Karibu atapata PhD na hatutaki kujua anasoma wapi na lini. Thank you!
Kwa ujasiri NAPE ni zaidi ya Mnyika kwasababu amweza kusimamia msimamo wake hata dhidi ya Katibu Mkuu wake makamba na waziri mkuu kutoka chama chake Lowasa. vitu ambavyo ni adimu kwa mnyika...na kama elimu itakuwa shahada NAPE ni zaidi ya Mnyika kwa mbali...lakini swali la msingi ni je, shahada peke yake ni kigezo mwafaka kuwalinganisha mnyika na Nape kwa mustakabali wa ubungo na taifa? au kuna zaidi? tujadilizaidi..hawa ni vijana muhimu sana, ni muhimu mmoja akaenda jimbo jingine ili wote wawili waingie mjengoni..,.inawezekana
He can not stand and argue like Mnyika ndio maana watu wanaquestion academic level yake. Ndipo ikawekwa kisaniisanii hapo juu yakaonekana ni yaleyale ya wanasisiem wenye PhD za vyuo visivyoeleweka. Anyway, whether alisoma Havard au Oxbridge he is incompetent before Mnyika. Mwekeni tuone muziki huo,tusiandikie mate bana!
Nadhani Achebe ametusadia wakati tukisubiri ya Mnyika nimepata miaka na vyuo alivyosoma Nape. Na kwakweli ni kati ya wanasiasa walosoma kwa kukaa darasani na sio online kama za 'ma Dr' flani tunaowajua. Na nimethibitisha na watu wa TUC, wanaohusika na uthibitishaji wa vyeti.Ni vizuri tukapata academic profile za wote, mnyika na Nape...hiyo ya Nape kweli tuoneshwe na miaka alochukua kama ambavyo na ya mnyika tutaoneshwa.