Jana nimeingia DSM kutoka kijijini kwetu Masasi na kufika Ubungo Stendi saa moja na nusu usiku. Nilichokikuta pale ni aibu, hakuna utaratibu kabisa kwenye kuingia na kupaki mabasi na magari madogo yanayokuja kuchukua abiria pale.
Pili nilifadhaishwa na jinsi ambavyo hawa watoa huduma hapa wamekazania kukusanya pesa kwanza kibabe na kwa maringo pasipo kujali uhuru na haki za watu wengine.
Nini kinaendelea hapa, mimi nilifikiri baada ya kurudi kwenye mikono ya serikali ya Jiji miundombinu na huduma nyingine zingeboreshwa lakini naona hakuna jipya zaidi ya kukomaa kwenye kukusanya ushuru kwa vita na mbwembwe
Na wewe kwanini uingie na ngalangala la masasi hadi ndani usiku wote huo ?? hukuona kituo njiani?
Na wewe kwanini uingie na ngalangala la masasi hadi ndani usiku wote huo ?? hukuona kituo njiani?
Ukweli serikali inatakiwa iwe makini na ifanye haraka kurekebisha mazingira ya pale, au mpaka mwekezaji?Ndiyo serikali yetu hiyo.huduma za jamii zote hazina afya nzuri.
Mkuu, UBT inasikitisha sana. Jiji wamesema wana-test kukusanya mapato wenyewe kwa 3 months ili wajue kituo kinaweza kuingiza kisasi gani. thereafter watafute operator.Ukweli serikali inatakiwa iwe makini na ifanye haraka kurekebisha mazingira ya pale, au mpaka mwekezaji?
Ni kweli Mkuu, seriously pale panatia kichefuchefu na sio mahala pana huduma njema tena. Kuna kitu hapa umeongea ni ukweli mtupuMkuu, UBT inasikitisha sana. Jiji wamesema wana-test kukusanya mapato wenyewe kwa 3 months ili wajue kituo kinaweza kuingiza kisasi gani. thereafter watafute operator.
Kinachinisikitisha ni kwamba, wale waajiriwa wa jiji sasa ndo wamekuwa balaa....ukitoa mia, wanachukua, ukitoa mia mbili wanachukua, kama kuna-popportunity ya kutokukupa receipt wanafanya hivyo. This means, mapato yataonekana ni madogo, hivyo wanampa operator ambaye atabid chini. BUT.....kwa vile wanaye JINI LIKUJUALO.....(Kinjeketile) watampa tena, kwani wataona kuwa yeye alikuwa analiingizia jiji hela nyingi kuloko matarajio yao.
Mchezo unakuwa umeisha kiivyo......Huwa natamani kutengeneza kiwanda cha hand grenade, then nilipue kila mla kodi yangu.
Ila utashangaa pesa ya hpo ndio ya kununua mashangingi mapya ya wakubwa-Unajua serikali yetu imekosa watumishi waadilifu na wenye nidhamu
Kimsingi ilitakiwa hela inayokusanywa hapo iwe ndo mtaji wa kukarabati stendi yenyewe,kulipa wafanyakazi wa hapo stendi na usafi kwa ujumla.Haihitaji akili nyingi kuifanya stendi ya ubungo kuwa na hadhi stahiki
Ila utashangaa pesa ya hpo ndio ya kununua mashangingi mapya ya wakubwa
Hata mimi inanikera sana kuona jiji kama hili ni chafu kila kona. Sasa nashangaa hata hapo kituoni ambako ni eneo liko chini ya usimamizi unaotambulika na eneo ambalo liko fenced bado kuna uzembe mkubwa vileMkuu,ndiyo maana unaona kila sasa Dar inatolewa kwenye list yakuwa among dirtiest cities in the world.Pia Meya wa jiji sijui kazi zao ni nini hasa
Hata mimi inanikera sana kuona jiji kama hili ni chafu kila kona. Sasa nashangaa hata hapo kituoni ambako ni eneo liko chini ya usimamizi unaotambulika na eneo ambalo liko fenced bado kuna uzembe mkubwa vile
mm nimeingia pale jana asubuhi sana..........wakati natoka, nimetoa 300 yangu, naona yule mama ananikodolea macho, kama vile ....si uende tu kwani unahitaji receipt? nikawa mkali, nikamwambia leta receipt hapa!
Jana nimeingia DSM kutoka kijijini kwetu Masasi.............................