A
Anonymous
Guest
Mtaani kwetu Ubungo, Makoka, DSM
Maeneo ya Kilimahewa kuna jirani amejenga nyumba ya kupangisha ambayo wanaishi wapangaji tu yeye anaishi mbali na hapo.
Sasa tatizo linaanza, choo cha hiyo nyumba kinavuja shimo la majitaka limeharibika hivyo majitaka yenye athari kwa mazingira na wakazi wa eneo hilo.
Cha ajabu akipelekwa Serikali za Mitaa hachukuliwi hatua wala nini na akirudi mtaani anaanza kusema mbovu kwa majirani kiasi cha kuleta uadui.
Tunaomba msaada kwa hili, kuna hatari ya kipindupindu na pia hata usalama kwa watoto maana shimo lipo wazi sana na bado linatumika.
----
JamiiForums imefanya juhudi za kuwasiliana na Mamlaka husika Manispaa ya Ubungo ambapo wamekiri kuna changamoto hiyo.
Joina Nzali Afisa habari Manispaa ya Ubungo ameiambia JamiiForums kuwa
Ni kweli kuna mwananchi alichimba shimo kwa ajili ya choo lakini hakumalizia kufunika na hivyo kujaa maji kipindi cha mvua. Baada ya wananchi kutoa taarifa, Afisa Afya wa kata ya Makuburi amemwandikia Notisi ya siku 14 inayomtaka amalizie ujenzi wa shimo hilo au kulifukia ili kuondoa kero hiyo. Asipotekeleza agizo hilo hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa
Notisi alipewa tarehe 17.06.2024 na itaisha tarehe 30.06.2024. Baada ya hapo manispaa itatembelea kuona utekelezaji wake kama hajatekeleza hatua nyingine za kisheria zitafuata