kamjabari
JF-Expert Member
- Mar 20, 2017
- 1,144
- 1,668
Kumekuwa na utiririshaji wa majitaka ovyo maeneo ya Ubungo Riverside kuanzia maeneo ya Msikitini mpaka Kituo cha Kaladala karibu na Riverside Bar kuna harufu kali inayosababishwa na maji taka yanayotokana na shughuli mbalimbali za Wakazi na Wafanyabiashara wa maeneo hayo.
Ambapo inadhaniwa pia kuwa kuna baadhi ya Watu wasio waungwana wanatiririsha taka za vyooni hasa kwa uwepo wa harufu mbaya na kali maeneo hayo.
Mfano ukitokea njia (barabara) ya Mchichani au Kibangu kupitia kwa Mama John Bar, kuna harufu inayo sababisha kukosekana kwa "oxygen" kwa maana ya hewa safi na ajabu pembezoni mwa barabara kuna huduma za maduka mbalimbali yakiwemo ya vyakula na watu wengi wanapita na kununua maeneo hayo.
Kuna wakati ukivuta hiyo hewa chafu unahisi kuuma kichwa na hata tumbo huku ukikosa amani na kupoteza tabasamu usoni.
Ni hatari kwa maisha ya Wakazi wenyewe, wapita njia, lakini ni hatari zadi kwa afya za wanunuzi wa bidhaa za vyakula maeneo hayo ambapo wauzaji wametamalaki mno maeneo hayo.
Kwani eneo hilo ni soko bubu ambapo majira ya jioni watu husheeni sana watokapo kazini na kurejea nyumbani, hupita maeneo hayo na kununua mahitaji mbalimbali na hasa vyakula.
Ushauri
Watu wa mazingira, Afya, Serikari ya mtaa huo na Wananchi kwa jumla wachukue hatua za haraka na makusudi ili kunusuru afya za Watu wa mtaa huo, mitaa jirani na wapita njia.
Hata hivyo miundombinu inayotumika kutiririsha uchafu huo ni muhimu kuangaliwa upya ikiwa ipo vyema kutiririsha maji taka bila kuwepo athali zinazoonekana sasa.
Kamjabari
Nawasilisha.🙏🏾
Pia, soma: Dar: Usafi wafanyika Ubungo Riverside. Manispaa ya Ubungo imewaomba TARURA na TANROAD kuzibua mitaro ya barabara