Ubunifu Tanzania/MAKISATU: VETA, COSTECH, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Waziri Prof. Mkenda, na Watendaji Wao, Wanastahili Pongezi za Dhati!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Screen Shot 2023-05-01 at 5.30.38 PM.png
Screen Shot 2023-05-01 at 5.30.58 PM.png

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Veta, licha ya kuwapatia Watanzania elimu ya ujuzi kama nia na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kuwezesha wananchi, hasa vijana kuajirika kwa urahisi, kuongeza tija ya uzalishaji viwandani na kuchangia vyema katika maendeleo ya nchi kiuchumi, VETA, imeibuka jambo kubwa kuliko, kushindanisha wahitimu wake katika mashindano ya umahiri kupitia siku inayoitwa VETA DAY, ambayo imeyangarisha Maonyesho ya Ubunifu Kitaifa yaliyofanyika Dodoma.

Oktoba, 2022 wakati akizindua Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera, Rais Samia alisema
“Tunazungumzia tatizo la kutokuwa na ajira, tunasomesha watoto lakini hawana ajira… Kazi yetu ni kuhakikisha tunawajengea uwezo vijana kwa kuwapatia ujuzi ili waweze kujiajiri na kuajiriwa,”

Na baada tuu ya kauli hiyo ya Rais, VETA ikaamua hakuna kulala.
Kwanza ikakamilisha kujenga kwa spidi ya umeme, vile vyuo ilivyokuwa kwenye ujenzi, na sasa VETA ina vyuo 50 vilivyokamilika vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi nchini Tanzania

Kisha ikaanza ujenzi wa vyuo vipya 33, ambapo vyuo 29, ni vya ngazi ya wilaya na vyuo ni 4 vya ngazi ya mkoa kuanzia Samia alipoingia ile mwaka 2022 hadi sasa mwaka 2023 na kazi inaendelea!.

Kazi hiyo kubwa na nzuri, imetumia Jumla ya Shilingi Bilioni 94.5 tuu ndizo zilizo tumika katika kuwezesha ukamilishaji wa ujenzi wa vyuo hivyo.

Sasa vyuo hivyo vinatarajiwa kuleta ongezeko la wanafunzi zaidi ya elfu 40 katika udahili kwenye vyuo vya VETA.

Moja ya sifa kubwa za VETA, sio tuu kutoa mafunzo mbalimbali ya ufundi stadi, bali pia ujenzi wa vifaa mbalimbali kwa matumizi, mfano kwenye hivyo vyuo vipya vyote, VETA imetumia jumla ya zamani mbalimbali 30,750 zilitengenezwa na VETA kwa ajili ya vyuo hivyo!.

Utekelezaji wa mradi huo wa uzalishaji samani za vyuo, umetoa ajira zaidi ya 15,000 kwa wananchi Watanzania na vyuo hivyo vitakapoanza kutoa mafunzo inatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 1000 za moja kwa moja.

VETA yatoa ujuzi kwa wananchi kwa ufadhili na ruzuku ya Serikali
Vijana wa Kitanzania wanaojiunga na mafunzo kwenye vyuo vya VETA wanalipa ada ya Shilingi 120,000 tuu kwa mwaka kwa wale wanaokaa bweni na Tshs 60,000 tuu kwa mwaka kwa wale wanaohudhuria mafunzo kwa kutwa kwa mwaka. Gharama zingine za mafunzo hulipwa kwa ruzuku ya Serikali.

Serikali ya Mama Samia, imeendelea kutekeleza programu mbalimbali za kuwawezesha wananchi wa makundi mbalimbali kujipatia ujuzi. Mfano kupitia Mpango wa Uanagenzi ulioratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) vijana zaidi ya 10,000 walimefadhiliwa kupata mafunzo katika vyuo vya VETA.

Hali ya uajirikaji wa wahitimu wa ufundi stadi

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha asilimia 75% ya wahitimu wa ufundi stadi wanaajirika mfano asilimia 32% ya wahitimu wa VETA, wame ajiriwa kwa ajira rasmi, huku asilimia 38% wakijiajiri.

Wahitimu wa VETA waliobaki ni ama wanajitolea, wanaendelea na masomo au wanafanya kazi kwenye karakana za familia.

VETA yafanya utambuzi, ukuzaji na uendelezaji Ubunifu
Ufundishaji na ujifunzaji wa ufundi stadi mara nyingi huchochea ubunifu. Mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA, yanawajengea walimu na wanafunzi utamaduni na ari ya kubuni teknolojia mbalimbali kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali katika jamii na kurahisisha shughuli za kiuchumi.

Hivyo VETA ikaamua kubuni mbinu ya kukuza ubunifu kupitia Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU), toka mwaka 2019 hadi mwaka jana, 2022 wabunifu 82 kutoka vyuo vya ufundi stadi na wabunifu 573 kutoka mfumo usio rasmi walitambuliwa, ambapo Shindano la Ubunifu siku ya VETA Day, limeyashamirisha sana Maonyesho ya mwaka huu ya Ubunifu Kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Uendelezaji ubunifu
VETA imekuwa ikisaidia uendelezaji wa ubunifu wa walimu na wanafunzi wa ufundi stadi, pamoja na wale walio katika mfumo usio rasmi kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na:

Kwanza ni kwa kuwaunganisha na kuwadhamini kupata ufadhili wa Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH). Kisha kuwawezesha kifedha kwa vyanzo vyake vya ndani, pamoja na kuwapatia nyenzo na vifaa kwa ajili ya kuendeleza ubunifu wao. Kisha kuzitangaza rasmi bunifu zao na kuwatangaza na kuwaunganisha na taasisi na mashirika mengine yanayosaidia uendelezaji ubunifu.

VETA kwa kushirikiana na wadau imekuwa ikitenga fedha na kuratibu uendelezaji wa wabunifu wa ufundi stadi.
Kupitia MAKISATU wabunifu 10 Bora wamekuwa wakiwekewa utaratibu wa kuendelezwa na Serikali kupitia COSTECH.

Hakuna nchi inayoweza kupata maendeleo bila Ubunifu wa kubuni bidhaa zake na kuzitumia kujiletea maendeleo ya kweli ambayo ni maendeleo endelevu. Hivyo ndivyo wenzetu wa ulaya ndio walioanza Mapinduzi ya Viwanda (Industrial Revolution), Marekani ikaja kuwapiku kwa teknolojia, China akaja kufunga kazi kwa kutengeneza kila kitu!.

Hivyo Tanzania tukiamua kwa dhati kukuza Ubunifu, iko siku tutatoka!.

Mungu ibariki Tanzania.
Paskali
 
Kwa kweli Hongera zao kwa Dhati!

Hatua kwa hatua, Kwata kwa kwata Tutafika....Inawezekana! Kazi Iendelee
 
Mada nzuri sana kwa mustkabali wa vijana wetu. Cha ajabu hakuna wachangiaji.
 
View attachment 2606361View attachment 2606362

ni maonesho sio maonyesho,ni kung'arisha sio kungarisha
 
Back
Top Bottom