Ubunifu wa Mamsampu Wangu Umezaa Matunda Sasa Anakula Kile Roho yake Inapenda

Dumelambegu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
1,052
Reaction score
257
Wandugu,
Mwenzenu niliugua ugonjwa wa ameoba kwa muda wa miezi kama mitano hivi. Kama baadhi mnaweza kujua kwamba ugonjwa huu, ukishaingia kutoka kwake ni kazi sana. Ilikuwa nakunywa dawa mara kwa mara lakini nikipima naambiwa bado amoeba ipo. Baadaye nilishauriwa ninywe dozi tatu mfululizo. Nilifanya hivyo na kupona lakini wakati natibu amoeba kumbe nilikuwa nasababisha madhara kwa "mzee" wangu. Ghafla nilishangaa mzee hanyanyuki na kushindwa kabisa kupanda mlima. Pamoja na jitihada za mamsapu wangu kumshikashika lakini wapi.

Kwa kweli wadau nilikosa raha. Nilijua udume wangu wa mbegu ndiyo umeishia hapo. Lakini siku moja mamsapu wangu katika pitapita yake alisikia kwamba supu ya kuku wa kienyeji iliyochanganywa njegere mbichi bila kuungwa chochote ni mlo muhimu sana kwa wanaume. Basi bila hata kuniambia chochote akaanza kuniandalia huo mlo kila asubuhi. Bahati nzuri mamsapu wangu ni mfugaji mzuri sana wa kuku wa kienyeji. Kila baada ya siku mbili au tatu ilikuwa lazima nipate hiyo menu. Nimefanya hivyo kwa mwezi mzima.

Baada ya wiki kama mbili hivi tangu nianze huo mlo tukiwa tumetulia kwenye 6x6 mamsapu wangu akaanza fujo zake. Nilishangaa sana kwani haukuchukua hata dakika mzee alisimama kwa hasira isiyo ya kawaida. Nilimpa haki yake mamsapu wangu na performance yangu siku hiyo ilikuwa no record tangu tuanze huo mchezo miaka takribani minane iliyopita. Kuanzia siku hiyo mpaka leo wikiendi zote angalau mara mbili au tatu lazima nipate supu ya kuku wa kienyeji iliyochanganywa na njegere mbichi. Kwa hiyo, wale wenzangu na mimi kama nanyi mmepitia mabonde na milima kama yangu, tafadhali anzeni kupata mlo huo. Unarejesha heshima ya Baba ndani ya nyumba.
 
eeh kumbe kuku wa kienyeji noma...ndio maana huwa hawaachi kuvukuzana mitaani
 
Ahaaa! Bora umenistua! Huyu baba ataisikia bombani supu ya kuku! Kumbe ndo kinachonitesa!

Hongera kwa kupona. Uache kula mikachumbari ya mtaani usipate tena amoeba.
 
Supu ya kuku na njegere tu? Lazima alikuwa anafanya mbinu mbinu
 

Na huo ni ubunifu, au naye alisikia kule kunako kamati ya ufundi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…