Nimekuwa kila nikipita maeneo ya masoko mengi yenye machinio ya kuku hapa Dar haswa Shekilango na Manzese ninarudishwa na harufu kali inayotoka kwenye machinjio hayo.
Cha kushangaza uongozi wa masoko hayo, serikali za mtaa na uongozi wa halmashauri zimekuwa kimya kabisa.
Kukiwa na mvua au manyunyu harufu ni kali ya uozo wa masalia ya kuku na damu.
Au hili tatizo naliona peke yangu? Viongozi wanapelekwa mbali humo hawafiki kabisa.
Mkuu nenda pale nyuki tegeta sokoni wanapochinjia kuku Kuna arufu na vumbi la ajabu Cha kushangaza wale jamaa wanaochinja wameshazoea hile hali na unakuta wameagiza chakula wanakula kule ndani Kuna siku niliingia Mle ndani nilipata mafua na homa kali.
Hiyo harufu hapo ni kali sana,damu zinatakiwa zijengewe chemba au shimo lifunikwe juu kwa zege,hiyo harufu hapo ni konki, halafu hao wanyonga kuku wamejazana kwenye hiyo kona nyuma ya kituo cha mafuta.