Uchafu ndani ya ndoa waendelea: Babu wa miaka 70 anaswa na mke wa mpangaji wake....mumewe aamua kusu

washwa washwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2012
Posts
1,613
Reaction score
723


SIKU chache zilizopita, gazeti moja maarufu hapa nchini liliripoti juu ya fumanizi la babu mwenye umri wa miaka 70, Rafael Mitasio aliyenaswa gesti akiwa na mke wa mpangaji wake.

Taarifa tulizozinasa zinadai kuwa mzee huyo amesusiwa mwanamke huyo.

Chanzo chetu cha habari kimedai kuwa, mara baada ya habari hiyo kutoka gazetini, mume wa mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina lababa Tausi aliumia sana hivyo akampa kisogo kitendo kilichomfanya mgoni huyo atangaze kumuoa.


“Ile habari ilipotoka kwa kweli mume wa yule mwanamke aliumia sana, akaamua heri huyo mzee amchukue kabisa kama ameona anaweza kumtunza kuliko yeye.

“Cha kushangaza yule mzee naye eti anadai wala habari hiyo haijamuumiza na anasema atamuoa kabisa mwanamke huyo ili kuwakata vilimilimi wabaya wake,”kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

Kufutia taarifa hizo, Mwandishi wetu alimtafuta baba Tausi lakini hakuweza kupatikana mara moja. Mzee Rafael alipotafutwa kuzungumzia kama kweli ana mpango wa ‘kumchukua jumla’ mwanamke aliyenaswa naye wakivunja amri ya sita, alizungukazunguka sana lakini mwisho akasema:

‘’Si mmeshaandika kuwa nimefumaniwa, haya kaandikeni tena kuwa nataka kumuoa kabisa ili mfurahi.”


Mzee Rafael aliripotiwa kufumaniwa hivi karibuni kwenye gesti ya Sekei iliyopo mjini hapa akiwa na mke wa mpangaji wake.


Tukio hilo liligeuka kuwa gumzo katika maeneo mengi ya mji huku wengi wakishangazwa na kitendo cha mzee huyo kumshawishi mke wa mpangaji wake mpaka wakanaswa wakiwa watupu gesti.


Hata hivyo, fumanizi hilo lilizua kizaazaa cha aina yake hadi likafikishwa polisi.
 
Dah! Najribu kufikiria huyo Babu alitumia gia gani kuchukua huyo mke wa mpangaji wake. Huyo mke hafai kabisa.
 
Ukishajijua hutimizi wajibu wako ndani kama mwanaume matokeo yake ndio haya. Unakuta mwanaume mwingine mbishi na mkorofi na mlevi hajui kutoa pesa ya kula nyumbani, unakuta kodi ya nyumba inapiga chenga,mwanamke anajinunulia nguo mwenyewe unategemea nini? lazima mwanamke atatafuta namna ya kuinusuru familia tu kuliko kufariki huku akijiona.
Wanaume angalieni hela ya matumizi mliyoacha nyumbani inalingana na misosi unayoikuta nyumbani?tafakari chukua hatua,wajibika.
 
mwambieni Baba tausi hiyo nyumba ahame mara moja km kashindwa mtafutia jamaa wakamtigo Babu Rafael Matisao
Halafu hiyo Guest ya Sekei ni wapi Arusha?
 
Huyu babu ni balozi wa nyumba 10 pale sekei Arusha, anafahamika sana kwa jina la "baba ana", mtoto wake mwingine anaitwa Eli (Ni wa kiume na tunaheshimiana naye sana). Nimewahi kuwa mpangaji wake kwa miaka miwili na hii ni tabia yake ya muda mrefu. Aliwahi kumtongoza mke wangu kwa ahadi lukuki...Wife aliponieleza tabia zake, sikumsemesha ila siku moja akateleza kwa jambo fulani...hapo nikamkumbusha na akahama kwake wiki moja na kutuma wazee waje kunitaka radhi.

Ki ukweli ni tabia mbaya sana katika jamii iliyostaarabika.....ila na huyu dada!!!! simpatii picha.
 
kama huyu babu mpaka leo bado anaendekeza alipotokea ujanawake sijui alikuaje yani hana haya
 
wanawake nikama kinyessi ikinyesha mvua kinaenda na maji yaani uwezo wakufikiri kwao ni mdogo sana huyu babu ninaimani hakutumia hata nguvu alichukua kilaini

aaahhaa! na mamako pia?
 
Hivi vizee havitumii nguvu sana, nahisi alimuahidi kumpa kodi ya chumba au nyumba mojawapo. Sasa wewe mwanamke huujui hata ule msemo usemao "Ukitaka kula haramu kula iliyonona"? Au babu ndo kanona? Ninahisi kama ungefumaniwa na kijana mtanashati kuliko mumeo, Mumeo angekusamehe na tangu hapo angeanza u-tanashati ili kukuridhisha. Sasa umeenda kwa babu, je mumeo ajizeeshe ili kukuridhisha? au akuache na kukurudia atakapo zeeka kama huyo babu? Umemtia aibu jamaa yangu
 
wanawake nikama kinyessi ikinyesha mvua kinaenda na maji yaani uwezo wakufikiri kwao ni mdogo sana huyu babu ninaimani hakutumia hata nguvu alichukua kilaini
mamaaaaaaaaaaaaa
 
Hapo kuna mambo mengi sana,labda jamaa hatekelezi wajibu wake wa matunzo,na kuwajibika sehemu zote!ama la huyu mama hana kazi ya kufanya wanashinda wote hapo nyumbani wameshazoeana sana na mizinga midogo midogo kwa mzee,akaona awe anamchuna tu,ila huyo baba angempiga na tigo kidogo aone tamu yake!!aibu sana kwa mzee kama huyo!
 
Mzee Rafael na Mama Tausi wana tabia sawa, hakuna wa kulaumiwa.
 
Hiki kibabuuuu!!jamani kilimfanya nini huyu binti!Vibabu vingine bwana,kilikuwa wapi miaka yote!
 

Mwambie huyo jamaa aliyeliwa aende Tanga au pale Segera tu atamkomesha huyo babu yaani vitu vyake vitatunguliwa na panya avione darini,
Kwani wana watoto wangapi? mpaka kamuacha watapata shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…