KERO Uchafu uliosambaa Manispaa ya Songea ni tishio Kwa afya zetu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
Sep 23, 2024
Posts
64
Reaction score
43
Hapa Manispaa ya Songea, ni kama viongozi wameweka pesa mbele kuliko kuwajali Wananchi kutokana na mazingira yalivyo.

Binafsi sijui wanazingatia nini au vigezo gani kumpa tenda mtu ambaye kazi haiwezi ya kukusanya taka na kusafisha maeneo mbalimbali ya Songea kwa kuwa moja ya changamoto inayoonekana ni kukosekana kwa vifaa vya kutosha kukusanya taka.
WhatsApp Image 2024-11-08 at 18.01.35_cb48dcfc.jpg

WhatsApp Image 2024-11-08 at 18.01.51_d5ac9c69.jpg
Ukitembea maeneo mengi kukuta uchafu umezaagaji katika maeneo tofauti ni kitu cha kawaida.

Mito: Mito inayotuzunguka imegeuzwa ni sehemu yakutupia takataka,mbaya zaidi Watoto wanacheza kwenye maji hayo yenye uchafu.

Nimeshuhudia hilo mara kadhaa mfano Wanafunzi wa Shule ya Msingi Majengo na Songea wapo jirani na mto ambao wanautegemea kwa kuchota maji yakumwagilia bustani za maua ya shule.

Mto huo umekuwa kama dampo la Manispaa, umejaa takataka na Walimu wanawatuma Wanafunzi wakachote maji hivyohivyo.

Wanafunzi hao wanasogeza taka kwa mikono bila kuwa na vifaa huku kukiwa na uchafu wa aina mbalimbali ikiwemo vinyesi vya Watoto kwenye pampasi zimetupwahumo na haja ndogo kwenye makopo humo.

Manispaa muwaonee huruma Watoto hawa, afya zao zipo mashakani wanachezea maji hayo kisha wananunua vitafunwa wanakula bila hata kunawa mikono.

Kinachofanyika ni hatari kwa afya zao kwa kiwango cha juu. Hapo wanakosaje magonjwa ya maambukizi?
WhatsApp Image 2024-11-08 at 18.02.13_e5eeeebb.jpg

WhatsApp Image 2024-11-08 at 18.02.16_61653f56.jpg
Mitaro: Mitaro imejaa takataka, watu wanatupa takataka kwenye mitaro na maeneo ya biashara,wafanyabiashara wanasafisha maeneo yao takataka wanatupia kwenye mitaro.

Majumbani nako wanachangishwa shilingi elfu moja kila familia kwa kila mwezi na bado takataka hazikusanywi mwisho wa siku zikizidi wanaamua kuondoa taka nyumbani na kwenda kutupa mtaroni au mtoni kwa wanaoishi karibu na mto.

Nyumbani: Wanalipa gharama ya usafi mara mbili,pesa zinazochangishwa na waliopewa jukumu la usafi na Manispaa na hawapiti kukusanya takataka hizo hadi wanaamua kuwalipa vijana wa mtaani waziondoe takataka hizo na wanaenda kuzitupa popote.

Mmomonyoko:Imekuwa kama Sheria sasa kila kwenye mmomonyoko kuwa sehemu ya kutupia taka kwa madai kuwa wanazuia mmomonyoko usiendelee.
WhatsApp Image 2024-11-08 at 18.02.21_b64fc8fd.jpg
Wananchi wanasema wanafanya hivyo kwa makusudi ili kuzuia mmomonyoko na kuhusu viongozi wao wa mtaa kuzuia wamejibu hawawazuii kwasababu nao wameona ndio njia sahihi ya kuzuia mmomonyoko.

Kinachotokea kipindi cha masika mvua ikinyesha maji yanatiririkia mtoni ambako Wananchi wanatumia maji hayo kwa kuoga, kufulia na kumwagilia mboga ziendazo sokoni.

Kwa ujumla Manispaa ya Songea tupo hatarini kupata madhara kiafya kulingana na maelezo ya daktari ambaye nimezungumza naye kuhusu hali hiyo:

1. Husababisha Magonjwa ya kuambukiza
Utupaji taka usiofaa unaweza kuvutia panya na wanyama wengine wanaoeneza magonjwa ya kuambukiza.

2. Utupaji Usio salama wa Makopo ya Kemikali zenye sumu
Kemikali zenye sumu kutoka kwa taka ngumu moja kwa moja zinachafua hewa, udongo na maji na hivyo kusababisha matatizo ya kiafya kama vile saratani, kasoro za kuzaliwa, na matatizo ya kuzaliwa.

3. Husababisha Magonjwa ya kupumua:
Taka za plastiki kutoka kwa utupaji wa taka zisizofaa zinaweza kuchangia magonjwa ya kupumua.

4. Husababisha majeraha yaliyosababishwa na taka zenye ncha Kali, utunzaji na utupaji wa vitu vyenye ncha Kali usiosalama unaweza kusababisha majeraha na kupelekea magonjwa kuambukiza.

5. Husababisha Magonjwa mengi:
Utupaji wa Taka usio salama husababisha kueneza Magonjwa yanayosababishwa na vimelea vya kuambukiza kama vile protozoa, minyoo ya vimelea na nematodi.

Kumbukumbua: Aliyekuwa Katibu Mkuu Afya –Prof. Abeli Makubi katika Toleo maalum la Oktoba hadi Disemba 2022 (huduma za afya na usafi wa mazingira) alisema;

“Lengo la Afya Mazingira na Usafi ni kukabiliana na kudhibiti kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza kama vile Ebola, UVIKO 19, Kipindupindu, Kuharisha na magonjwa yatokanayo na athari za kemikali na mionzi kwa kudhibiti visababishi vya afya mazingira na usafi.

Aidha, afya mazingira na usafi husaidia kukuza ustawi wa jamii kwa kuweka maeneo yanayozunguka jamii kuwa nadhifu. Afua hii hujumuisha udhibiti wa taka, udhibiti wa uchafuzi wa mazingira, usalama wa chakula maji, usalama wa afya mahala pa kazi, ujenzi wa vyoo bora na matumizi pamoja na tabia chanya za usafi katika jamii”.

Maoni yangu nadhani kwanza mkawanusuru Watoto wetu wa shule ya msingi Majengo na Songea. Pili halmashauri ongezeni vitendea kazi kama vile magari ya kubeba taka na muwasimamie mliowapa tenda sio kukaa tu ofisini kusubiri pesa na kingine wekeni basi vitupia taka pembezoni mwa barabarani, Wananchi tunaishi mazingira machafu sana na masika ndio hiyo.
WhatsApp Image 2024-11-08 at 18.02.22_38734b05.jpg

WhatsApp Image 2024-11-08 at 18.02.37_ef8a6c78.jpg

Uchafu uliosambaa Manispaa ya Songea ni tishio kwa usalama wa Watoto

Hapa Manispaa ya Songea,ni kama viongozi wameweka pesa mbele kuliko kuwajali Wananchi kutokana na mazingira yalivyo.

Uchafu ni tabia, ukiona mji ni mchafu basi huyo kiongozi wake huenda hata huwa hafui kitasa chake
 
Ndio maana mito inachungwa sana ila huu sijui kwanini wameacha mpaka ifikie hali hiyo
Uchafu ni hulka ya watu hapo inatakiwa mkuu wa Mkoa au Wilaya mkorofi au mwenye nidhamu kuwanyoosha hawa wachafu
Kama Aggrey Mwanri alihakikisha mkoa wa Tabora kila mmoja anapanda miti na usife itakuwa uchafu huo?

Mnataka watu kama hao
 
Hao viongozi wanachojali Pesa kutoka Kwa mzabuni inaingia basi kufuatilia Kama taka zinakusanywa aaanha
 
Back
Top Bottom