Uchafu vyuo vikuu Tanzania ni athari ya utandawazi au ndio usomi?

Mlombo

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2013
Posts
243
Reaction score
49
Ndugu wanajukwaa hali maadili ya sasa katika vyuo vikuu vyetu vya uma na vile vya binafsi inazidi kuwa mbaya huku watoto wa kike wakitembea nusu uchi na kuranda randa katika kumbi za starehe,kwa mujibu wa utafiti nilioufanya kwa kutembelea vyuo kadhaa hapa nchini,taaluma imeporomoka kwa asilimia 30 ukilinganisha na miaka ya 1980.

Je ni kweli kua kuanguka kwa taaluma ni zao la kuporomoka kwa maadili?kama ni kweli kuna haja yoyote ya serikali kuingilia kati suala la maadili na kutunga upya sheria zinazopunguza uhuru wa mwanachuo?je mfumo wa kimaadili katika vyuo vikuu vyetu vya umma na vile visivyo vya umma kuna haja yoyote ya kuufanya kama ule wa vyuo vya ualimu?au waendelee na mfumo wa sasa wa udhibiti wa maadili?au vyuo viige mfumo wa kile chuo cha waislam cha morogoro ambacho tunakisikia wazazi na waume wenye wake zao wakikisifia kwa namna kinavyo dhibiti suala la maadili na kulinda utamaduni wa mtanzania?

Nini mtazamo wako katika hili,tukiache kizazi kiteketee kwa utamaduni wa kimagharibi na kuingia na viroba Darasani au tandamane kuishinikiza serikali kulichukua hili ka ma janga la kitaifa?AU VITENDO VYA ULEVI,KUA NA BOY/GIRL FRIEND,UKAHABA VIMINI NA KATA K,n.k ndio vigezo vya usomi?
 
Hakuna cha maadili hapa!!! hata viongozi wa CCM wanaongea hovyo tuuuuuu.. maadili,maadili maadili kumbe uizi mtupu! . ANYWAY: Mimi naona kama hamna haja ya serikali kupambana na maadili, badala yake ipambane na uchumi maana tunafuata maadili ya tulio nyuma yao kiuchumi. Usiwe kama wale ma RPC wa temeke na kinondoni wanaotumia vyeo vyao kupambana na mambo ya kijinga!!!! kama ni maadili na utamaduni hatuna yetu tunayo yasimaamia tena. " ideally, we must be behind those infront us" kuelewa hili wala halihitaji Calculator. Kwaheri.
 
Mods naomba muhamishe huu up.u.u.zi, hana jipya analolisema huyu, haujui msingi wa maadili unaanzia nyumbani, yeye aache kulea watoto na kuwafundisha maadili ategemee kuandamana ili serikali ifundishe maadili kwa watoto wake, huu si -----?
Katika hiyo research yake aligundua nin kilichoshusha hiyo taaluma?
Hao waliosoma miaka ya 80 mbona hakuna chochote cha maana wanachofanya?
Wataalamu wote wanatoka nje?
Hata vijiti vya kuchokonolea meno tunaimport toka china?
Elimu yao iliyokuwa bora wana nini wamefanya nayo?
Kila kona ya nchi tunakutana na wataalamu wa china na wahindi!
Nyie mliosoma miaka hiyo mmebahatika kuwa wauwaji wa viwanda, mafisadi, bongo lala, hakuna jipya mnalofikiria, hakuna uvumbuzi wa jambo lolote mlilofanya..
 
'Mawazo ya mtu ndio rubani wake'..by Mama yangu mzazi(rest in peace). Nenda kachape kazi mkuu huwezi kuzuia hii evolution hata ndani ya familia yako.
Kuna makubwa ya kufanya kuliko haya.
 
Upo sahihi,,kuna haja ya kuangalia mifumo ya vyuo vikuu Uozo ni mwingi
 
Upo sahihi,,kuna haja ya kuangalia mifumo ya vyuo vikuu Uozo ni mwingi
Njia mojawapo ni vyuo husika kuweka sheria kali na kuzitekeleza.
 
Hadi sasa na tangu uwepo wa vyuo vikuu na ongezeko lake ni kuwa kumekuwepo na matukio mengi sana ya ajabu ajabu ya kimaadili. Kuweka picha za uchi mtandaoni, na uwepo wa mambo mengi ya aibu yasokuwa na dhima ya kijamii hasa pale tunapoiona hii jamii inayotakiwa kuja kuliendeleza taifa hili kwa wasomi hwa wajinga.

Tunajifunza nini? kama hawajitambui na wapo chuo kikuu tuwasaidieje? Je walioko shule za msingi na sekondari wafanye nini au wajifunze nini?
 

mungu atusaidie
 
iwekwe sheria kama ya usafi, mfano, ukitipa uchafu unafagia mji mzima au unatoa fedha kibao. Vyuoni wangekuwa wanabakwa (mtungo) au fimbo 20 akikutwa hayupo kimaadili. Hahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…