Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 144
SALIM SAID SALIM
RIPOTI ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa mwaka 2007/08 ilieleza kuwa zaidi ya sh milioni 100 (nyingi sana kwa Zanzibar) zilitumika visivyo halali katika idara na taasisi mbalimbali za serikali.
Katika ripoti hiyo yenye maelezo ya kusikitisha na kutisha, iliyowasilishwa katika kikao kilichopita cha bajeti cha Baraza la Wawakilishi, ilielezwa kuwa baadhi ya maofisa wa serikali walitumia vibaya fedha za umma na hawajali taratibu ziliowekwa za matumizi ya fedha za serikali.
Ripoti hiyo ilieleza kwamba rasilimali nyingi za serikali zilikuwa hazijulikani zilipo na nani alizichukua haifahamiki na baadhi ya taasisi ziligunduliwa kuwa na magari mengi, nyumba na mashamba bila kuwapo kumbukumbu rasmi za mali hizi. Bila shaka hali hii hutoa mwanya kwa wajanja kuiba mali za serkali.
Alipowasilisha ripoti hii ambayo nakala zake zilikuwa chache (sijui kwa nini), lakini naamini ni kielelezo kingine cha kutokuwapo uwazi katika SMZ, japokuwa viongozi wake hununa unapowaambia, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba na Utawala Bora, Ramadhani Abdulla Shaaban, alisema kulikuwapo na matumizi ya mamilioni ya shilingi yaliyokosa vielelezo.
Mkaguzi pia aligundua kuwapo kwa dola 70,895 za Marekani bila maelezo ya kuwapo kwa fedha hizo. Vile vile palikuwapo vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 160, ambavyo ununuzi wake hauna uthibitisho wa stakabadhi. Hapa panazuka mashaka kwamba ulitumika ujanja katika ununuzi huo na wapo watu waliofaidika na nchi kufisidika.
Unapoitafakari ripoti hii ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali unaona wazi kuwapo kwa vitendo vya ufisadi na rushwa katika baadhi ya idara na taasisi za Serikali ya Zanzibar ambavyo vinahitaji kufuatiliwa kwa undani zaidi na hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wahusika wa uovu huu. Vile vile kutopatikana kwa urahsi kwa ripoti hiyo ni kielelezo kwamba SMZ inaendesha shughuli zake kwa siri.
Zanzibar ni maskini. Kwa muda mrefu imekuwa na matataizo ya fedha si tu kwa miradi ya maendeleo bali hata kwa kutoa huduma muhimu za kijamii, kama matibabu, maji na elimu.
Kinachoonekana ni kwamba kwa muda mrefu SMZ imewafumbia macho wahujumu uchumi kwa sabbu zisioeleweka. Miaka miwili iliyopita tuliambiwa waligunduliwa wafanyakazi hewa 5,000 katika utumishi wa serikali, hata ndani ya vikosi vya SMZ.
Katika baadhi ya sehemu wafanyakazi hewa walilipwa mishahara kwa karibu miaka mitano. Huu ni ujambazi wa hali ya juu, bila shaka ulikuwa mtandao mchafu wa wajanja wachache waliojipatia kirahisi fedha za umma na kujenga majumba ya kifahari na wanasomesha na kutibu watoto wao nje ya nchi.
Watu hawa hawakuwaonea huruma watu maskini wa Zanzibar wanaopata shida za maisha, ikiwamo kukosa dawa muhimu wanapofika hospitalini. Hali hii imechangiwa na wizi wa fedha kidogo zilizopo Hazina, unaofanywa na mafisadi wachache.
Kilichofanyika baada ya kutolewa ripoti juu ya wafanyakazi hewa ni kwa maofisa wachache wa ngazi za chini kufunguliwa mashitaka.
Kinachoshangaza ni kuwa hakuna hata mkubwa hata mmoja aliyewajibishwa wakati wao ndio wadhamini na wasimamizi wakuu wa idara, taasisi na vikosi. Kama fedha si miongoni mwa mambo wanayoyasimamia sijui wanasimamia nini!
Wakati umefika wa kuachana na propaganda zisizo na manufaa, za kusema viongozi na watendaji wa SMZ ni safi, hawana dosari na unaweza kusema ni kama malaika na hakuna rushwa wala ufisadi srikalini.
Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa SMZ imeonyesha uchafu uliopo katika idara na taasisi zake. Kinachotakiwa ni kuifuatilia kwa karibu hii ripoti ili kukomesha mwenendo huu mchafu wa kutumia vibaya fedha za umma na mali za serikali ambazo wapo wanaoona ni haki yao kuzipora watakavyo.
Mwenendo wa utendaji kazi wa wakaguzi wa ndani wa fedha waliopo katika idara na taasisi mbalimbali za seikali unapaswa kuangaliwa au kuundwa upya ili hawa wakaguzi wawe na sauti na waweze kusaidia kupunguza wizi na ubadhirifu wa fedha na mali za serikali.
Kama wakaguzi wa ndani wa hesabu katika idara za serikali wangekuwa na sauti, wanafanya kazi zao kwa uadilifu na kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na kukataa kufumbia maovu wizi wa aina yoyote ile huu upoteaji wa fedha za serikali uliolezwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali usingefikia kiwango cha kutisha kilichoelezwa.
Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu ya Serikali imeonyesha kuwapo mafisadi katika SMZ na si vizuri kudanganyana. Wakati ni huu wa kuwasaka kwa uvumba na ubani na kuwawajibisha kisheria badala ya kila siku kuona wanaoshitakiwa kwa wizi ni wale wanaotembea miguu chini, ambao wameiba nazi mbili, fungu la muhogo au mandazi.
Hawa wanaoiba ndizi au mandazi ni vijizi vidogo vinavyofanya hivyo kutokana na njaa inayowasumbua. Wezi hasa ni hili kundi la maofisa wachache serikalini ambao wanachota bila woga mamilioni ya shilingi na kutusukuma kutoka kwenye umaskini na kutupeleka kwenye ufukara uliokithiri.
Hawa ni watu hatari sana, ambao hawafai hata kidogo kuonewa haya, muhali wala huruma, hasa kwa vile hawana utu, imani wala hisani na hawajali kuona wananchi wenzao wanateseka kutokana na wao kupora fedha umma. Tuwasake mafisadi kwa nguvu zetu zote za kisheria ili tuinusuru nchi yetu na hawa mafisadi kabla hawajatoa roho zetu na za watoto wetu.
SOURCE: TANZANIA DAIMA.