Uchafuzi wa hewa wasababisha vifo zaidi ya milioni 8 duniani kote mwaka 2021

Uchafuzi wa hewa wasababisha vifo zaidi ya milioni 8 duniani kote mwaka 2021

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Ripoti mpya ya kina inayoonesha athari hasi ya hewa chafuzi kwenye afya imetolewa leo nchini Marekani huku ikiweka bayana kuwa uchafuzi wa hewa umeibuka na kushika nafasi ya pili duniani kama kihatarishi kinachoweza kusababisha kifo.

Ikipatiwa jina Hali ya Hewa Duniani au SoGA ripoti imetolewa katika majimbo ya Massachussets na New York nchini Marekani na taasisi ya Health Effects au HEI kwa ushirikiano kwa mara ya kwanza na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.

SoGA inasema mwaka 2021 watu zaidi ya milion 8 walikufa kwa sababu ya hewa chafuzi. Ripoti inasisitiza ongezeko la madhara zaidi ya hewa chafuzi kwa afya ya wakazi wa dunia na kwamba imezidi hata tumbaku na lishe duni kwenye uwezekano wa kusababisha vifo.

Ikiangazia watoto, ripoti inaonesha jinsi hewa chafuzi inavyoathiri vibaya watoto kwani takwimu za mwaka 2021 zinaonesha kuwa zaidi ya watoto 700,000 waliokuwa na umri wa chini ya miaka mitano walikufa kwa kuvuta hewa chafu.

“Hii ina maana hewa chafuzi imezidi hata hatari ya mtoto wa umri huo kufa kwa utapiamlo. Moshi wenye hewa chafu ndani ya nyumba, utokanao na kupika kwa kutumia nishati inayochafua hewa umeripotiwa kusababisha vifo vya watoto 500,000 kati ya hivyo 700,000 hasa barani Afrika na Asia,” imesema ripoti hiyo.

United Nations
Habari za UN

AUDIO AND SUBSCRIPTION
KABRASHA LA SAUTI
SAJILI

Uchafuzi wa hewa wasababisha vifo zaidi ya milioni 8 duniani kote mwaka 2021. Uwepo wa magari mengi ya umeme kutamaanisha uchafuzi wa hewa utapungua na mazingira yatakuwa bora zaidi.

IMF/Crispin Rodwell Uwepo wa magari mengi ya umeme kutamaanisha uchafuzi wa hewa utapungua na mazingira yatakuwa bora zaidi.
19 Juni 2024Afya
Sasa uchafuzi wa hewa ni sababu ya pili kwa kusababisha vifo
Yapita tumbaku na lishe duni
Miongoni mwa waliokufa kwa hewa chafuzi ni watoto wa umri ya chini ya miaka 5
Kupikia kuni na mkaa ndani ya nyumba ni moja ya visababishi
Ripoti mpya ya kina inayoonesha athari hasi ya hewa chafuzi kwenye afya imetolewa leo nchini Marekani huku ikiweka bayana kuwa uchafuzi wa hewa umeibuka na kushika nafasi ya pili duniani kama kihatarishi kinachoweza kusababisha kifo.

Ikipatiwa jina Hali ya Hewa Duniani au SoGA ripoti imetolewa katika majimbo ya Massachussets na New York nchini Marekani na taasisi ya Health Effects au HEI kwa ushirikiano kwa mara ya kwanza na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.

SoGA inasema mwaka 2021 watu zaidi ya milion 8 walikufa kwa sababu ya hewa chafuzi. Ripoti inasisitiza ongezeko la madhara zaidi ya hewa chafuzi kwa afya ya wakazi wa dunia na kwamba imezidi hata tumbaku na lishe duni kwenye uwezekano wa kusababisha vifo.

Ikiangazia watoto, ripoti inaonesha jinsi hewa chafuzi inavyoathiri vibaya watoto kwani takwimu za mwaka 2021 zinaonesha kuwa zaidi ya watoto 700,000 waliokuwa na umri wa chini ya miaka mitano walikufa kwa kuvuta hewa chafu.

“Hii ina maana hewa chafuzi imezidi hata hatari ya mtoto wa umri huo kufa kwa utapiamlo. Moshi wenye hewa chafu ndani ya nyumba, utokanao na kupika kwa kutumia nishati inayochafua hewa umeripotiwa kusababisha vifo vya watoto 500,000 kati ya hivyo 700,000 hasa barani Afrika na Asia,” imesema ripoti hiyo.

UNDP inasema kufikia nishati salama ya kupikia kunahitaji majawabu yanayoshirikisha jamii yenyewe.UNDP Zimbabwe UNDP inasema kufikia nishati salama ya kupikia kunahitaji majawabu yanayoshirikisha jamii yenyewe.
Janga la afya duniani
Ikiwa imetumia pia takwimu za ripoti ya Mzigo wa Magojwa duniani yam waka 2021, ripoti inachambua zaidi madhara ya vichafuzi vilivyoko kwenye hewa kama vile chembechembe ndogo zaidi za hewa chafuzi au PM2.5, ambayo si rahisi kuibaini kwa macho, hewa ya Ozoni au (O3), naitrojeni dioksaidi (NO2), na moshi ndani ya nyumba katika zaidi ya nchi 200.

Ripoti inabainisha kuwa chembe chembe hizo ndogo zimesababisha zaidi ya asilimia 90 ya vifo vyote zaidi ya milioni 8 duniani.

“Chembe chembe hizi ni ndogo mno kiasi kwamba zinaweza kuingia moja kwa moja kwenye mapafu na mfumo wad amu na kusababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile magonjwa ya moyo, kiharusi, kisukari, saratani ya mapafu na moyo kushindwa kufanya kazi,” imesema ripoti hiyo.

Rais wa HEL, Dkt, Elena Craft akizungumzia ripoti hiyo amesema “tunatumai SoGA itatoa taarifa na hamasa ya mabadiliko. Hewa chafu ina madhara makubwa kwenye afya. Tunafahamu kuwa kuhakikisha kuna hewa safi na kuboresha afya ya umma ni mambo yanayowezekana na yanaweza kufanikiwa.”

Ripoti pia inachambua uhusiano kati ya uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabianchi ikisema kwamba chembe chembe hizo ndogo aina ya PM2.5 ni matokeo ya kuchoma nishati kisukuku, viyoyozi vya kwenye makazi, mitambo ya makaa ya mawe, shughuli za viwanda na mioto ya nyika.

Utoaji wa hewa hiyo unapunguza ubora wa hali ya hew ana inachangia katika mabadiliko ya tabianchi kwa kutoa hewa chafuzi.

Matokeo yake, jamii zilizo hatarini zinabeba mzigo wa hea chafuzi na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa mara ya kwanza ripoti imechunguza madhara ya hewa ya NO2 au Naitrogeni Daioksaidi kwenye ugonjwa wa pumu kwa watoto.

Hewa hii chafuzi inatoka kwenye magari na huathiri kwa kiasi kikubwa wakazi wa mijini, hasa kwenye nchi za vipato vya juu.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Kitty Van Der Heijden anasema licha ya maendeleo katika afya ya mama na mtoto, kila siku takribani watoto 2,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano wanakufa kutokana na madhara ya afya yasababishwayo na uchafuzi wa hewa.

“Kutochukua kwetu hatua kuna madhara makubwa kwa kizazi kijacho, kwenye afya yao na ustawi wao. Udharura wa jambo hili haukwepeki. Ni vema serikali na sekta ya biashara wazingatie takwimu hizo na wazitumie vema ili kupunga uchafuzi wa hewa na kulinda watoto.”

Source UN News
 
Back
Top Bottom