Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Siku za karibuni kumekuwepo mlipuko (outbreak) ya matumizi mabaya ya maneno ya lugha ya Kiswahili katika majukwaa ya JF. Inaonekana ima watu wanaigana katika kuandika vibaya au hawajui wanaiga nini. Inawezekana anayeandika ni mtu mmoja akiwa na ID tofauti
Ladha ya lugha ni kutamkwa na kuandikwa kama ilivyo. Wapo waliozaliwa maeneo ambayo Kiswahili si lugha ya asili. Mmoja wa watu hao ni Mh Shibuda anayezungumza lugha nzuri sana ya Kiswahili licha ya kutoka mikoa ya kati, hajaathiriwa na herufi 'r'
Ni kama Mwalimu Nyerere aliyeongea Kiswahili kizuri sana licha ya kutoka mkoa kanda ya Ziwa.
Naomba niweke baadhi ya maneno yanayotia kinyaa na kutumika hovyo
JIRI na JILI Sahihi ni MSAJILI siyo MSAJIRI
RAU na LAU Sahihi ni DHARAU siyo DHALAU
URI na ULI Sahihi ni USHAURI siyo USHAULI, JEURI siyo JEULI
SIRI na THILI Sahihi ni KITHIRI siyo KISIRI, MITHILI siyo MITHIRI
BURI na BULI Sahihi ni KIBURI Siyo KIBULI
RI na LI Sahihi ni LIPUA Siyo RIPUA
PERE, PELE Sahihi ni PELEKEA Siyo PEREKEA
Hebu fikiria habari kama hii itakavyokutia maudhi ;
'' Msajiri na mkuu wa taaruma wamekubariana kushugurikia suara la mishala na masirahi ya wanachuo na watumishi.
Makamu mkuu amesema maandamano yamekisiri na kuasiri sana shuguli za taaruma.
Hivyo, ni muhimu jamii ya chuo ikae na kutoa ushauli nini kifanyike.
Majadiliano yasiwe na dhalau mithiri ya watu waliochanganyikiwa.
Vulugu zitaperekea kuhalibu usarama na amani ya chuo na hatua kari zitachukuriwa kwa wausika
Chuo hakitavumuria kibuli cha watu na watakaokaidi watakuwa wamejiripua wenyewe na kuperekea kupoteza usajiri wao katika chuo.
Shukulani sana''
Hayo ni baadhi ya maneno machache sana, niseme kuna matumizi ya ''RI' mabaya , yanatia kinyaa na kuharibu utamu wa lugha. Hakuna anayeweza kusema anamuda lugha kwa asilimia zote, hata hivyo yapo makosa ya wazi yasiyofaa kutendwa. Yanaudhi , yanatia karaha na kukihirisha. Hata kama lafudhi yako inakuelekeza vile ni lazima ukidhi haja ya lugha hivi.