Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hapa ni katika kata ya Usagara, kijiji cha Nyangh'omango,kitongoji Nyaruhama kuna uchafuzi wa mazingira unaendelea eneo hili kwa kuchimba moramu eneo last makazi ya watu.
Hili jambo linahatarisha maisha kwa wakazi wa eneo hili hasa watoto, shimo ni refu sana wakati wa mvua maji hutuama humo jambo ambalo ni hatari sana maisha ya watu eneo hili.
Mkuu wa wilaya ya halmashauri ya Misungwi, Mkurugenzi wake watu wa madini, Ardhi na Nemc tunaomba msitishe zoezi hili mara moja na hili shimo lifukiwe na viwanja via watu walioathirika na kulika sababu ya hilo shimo wapate haki yao.
Pia viongozi wa kata mpaka kitongoji wawajibishwe kwa kuruhu hiyo shimo kuchimbwa katikati ya makazi ya watu.