Uchafuzi wa Mazingira

Columbus

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
2,002
Reaction score
651
Nimekuwa na dhana tofauti juu ya uchafuzi wa mazingira, viongozi wetu wamekuwa wanatoa miongozo mbalimbali ya utunzaji wa mazingira na athari ambazo zinaweza kuletwa na uchafuzi wa mazingira. Kumekuwa na kampeni mbalimbali ambazo lengo lake ni kuboresha mazingira tunayoishi na yale yanayotuzunguka.
Hivi karibuni nilimsikia kiongozi mmoja akizungumzia utaratibu mpya wa kutunza mazingira. Alitoa mwongozo kwa watoa huduma za mabasi yanayosafiri mwendo mrefu, alisema kuanzia sasa abiria hawataruhusiwa kuchimba dawa wakiwa safarini isipokuwa katika sehemu maalumu. Kwa mtazamo wangu mwongozo huu niliuona kama ni wa kupotosha hali halisi ya uchafuzi wa mazingira.
Kisayansi unapojisaidia maporini iwe ni mkojo au haja kubwa ni wazi unasaidia kutunza mazingira kwa sababu mimea au uoto wa asili huboreka na kustawi kama vile wafanyavyo wanyama wengine huko msituni. Ingalikuwa mwanadamu anatupa taka za sumu kama mafuta ya diesel au bidhaa zingine za petrol ningaliamini kuwa huo ungekuwa ni uchafuzi wa mazingira.
Kwa hali hii naona suala hili limekuwa na usiri fulani, yawezekana maamuzi haya yalikuwa yamelenga manufaa ya watu fulani na sio kweli kwamba kwa kujisaidia porini unakuwa unachafua mazingira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…