AljuniorTz
JF-Expert Member
- Jan 6, 2009
- 544
- 18
Kama mfungwa anaweza akapata nafasi ya kusoma hadi kutunukiwa digrii akiwa gerezani, itashindikanaje kura?Wananchi wenzangu kuna suala nahitaji tuliangalie kwa uzito wake; je ktk uchaguzi wa mwaka huu wafungwa watapiga kura kuchagua rais, wabunge na madiwani?
Mwanzoni mwa mwaka huu nilibahatika kutembelea gereza fulani hapa nchini; ktk mazungumzo yetu (nilikuwa na baadhi ya staff members) na mkuu wa gereza tulimuuliza suala la wafungwa na kupiga kura kuchagua viongozi wa nchi; akatujibu kuwa suala hilo lipo ktkt mchakato na kuna uwezekano mkubwa sheria ikapitishwa ili waweze kupiga kura ktk uchaguzi wa mwaka huu.
je hii sheria ilipita? wenye habari zaidi watujuze
Wananchi wenzangu kuna suala nahitaji tuliangalie kwa uzito wake; je ktk uchaguzi wa mwaka huu wafungwa watapiga kura kuchagua rais, wabunge na madiwani?
Mwanzoni mwa mwaka huu nilibahatika kutembelea gereza fulani hapa nchini; ktk mazungumzo yetu (nilikuwa na baadhi ya staff members) na mkuu wa gereza tulimuuliza suala la wafungwa na kupiga kura kuchagua viongozi wa nchi; akatujibu kuwa suala hilo lipo ktkt mchakato na kuna uwezekano mkubwa sheria ikapitishwa ili waweze kupiga kura ktk uchaguzi wa mwaka huu.
je hii sheria ilipita? wenye habari zaidi watujuze
Sio Tanzania ya leo, labda baada ya miaka 15 ijayo. Watanzania waliopo nje ya nchi hawaruhusiwi kujiandikisha na kama hawajajiandikisha hawawezi kupiga kura. Wengi waliopo huko wanaitangaza tanzania kwa kila hali na wengine wanafanya kazi za serikali lakini hawapewi fursa hiyo.
Ukiuliza kwa nini hawaruhusiwi hakuna jibu utakalopata zaidi ya kuambiwa kuwa mchakato unaendelea. Mchakato unaendelea Kivipi ? hakuna atakayekujibu.
Hakuna sheria ya mfungwa kupiga kura ingawa kupiga kura ni haki ya msingi kwa kila mtu pamoja na mtu aliyekosa na au aliyetuhumiwa ( mahabusu) na bahati mbaya siku ya uchaguzi atakuwa mahabusu. Watanzania walio nje hata wanaotumikia serikali yetu hawatapiga kura. wanaosoma na walioenda kwa biashara pamoja na wagonjwa wote watakosa haki hii.
Wanaoweza kujibu ni mwanasheria mkuu wa serikali na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi
Tunaweza kusema hizi ni mojawapo ya changamoto kwa wapinzani wanatakiwa wawepo kwa wingi bungeni ili kuwezesha kubadilisha sheria hizi za kibaguzi na zinazokinzana na sheria mama (katiba) ambayo inasema kila raia ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa...