muonamambo
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 875
- 545
Nimekuwa nafuatilia kwa ukaribu chaguzi mbalimbali Tangu zile za 2005 na 2010 na kuona mbinu chafu zinazotumiwa na chama Tawala CCM tangu wakati wa kampeni, kwenye tume ya uchaguzi, wakati wa kupiga kura na hata kutangazwa kwa matokeo. Mbinu hizi zikiwa pamoja na kuwaenguwa wapinzani kwa kusingizia sio raia, kuchelewesha kufungua kwa vituo, kurubuni mawakala, kupenyeza kura zisizo halali, kutishia wapiga kura, kushinikiza tume za chaguzi kutangaza matokeo ya uongo nk.
Napotazama muelekeo wa siasa na kuanza kwa kampeni mapema zaidi na kuonekana kutokukubalika kwa chama tawala; hasa baada ya kuacha kazi ya msingi ya kuwaletea Watanzania maendeleo na kujikita kwenye siasa mapema zaidi kabla ya wakati wa uchaguzi. Napata mashaka kama CCM watakubali matokeo ikitokea kuwa wameshindwa kama walivyo fanya chaguzi zilizopita.
Nipeni maoni yenu wana JF je mnadhani CCM watakubali matokeo kirahisi pale watakaposhindwa?