Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020 hauwezi kuwa wa Huruvna Haki bila kushiriki kikamilifu

Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020 hauwezi kuwa wa Huruvna Haki bila kushiriki kikamilifu

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Ninaandika hoja hii ili kuibua mjadala wa wazi kuhusu dhana ya Uchaguzi Huru na Haki

Ili kuelewa hasa kuhusu uchaguzi HURU na HAKI ni lazima tuelewa dhana ya Uhuru na Dhana ya haki

Nianze na kuelezea UHURU-Ni hali ya kuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote lile bila kuingiliwa wa la kuzuiwa kwa kuzingatia kwamba jambo hilo haliingilii uhuru wa mwingine.Kwa dhana hii basi uhuru wowote ule lazima uwe na Mipaka.

HAKI ni hali ya kuonekana kwamba kila mmoja anatendewa kwa kadiri anavyostahili kwa kuzingatia uwezo wake.nafasi yake na zaidi kwa kuzingatia utu wake na bila kuvunja uhuru wake.

Kwa mujibu wa maelezi yangu haya unaona kabisa kwamba UHURU na HAKI viategemeana kwani ili HAKI itendeke lazima kuwe na uhuru na ili uhuru uwepo lazima haki izingatiwe.

Kwa hivyo basi kama UHURU upo basi HAKI nayo ipo .

Sasa nirudi kwenye uchaguzi.Katika Uchaguzi UHUR na HAKI lazima vizingatiwe katika kila hatua kuanzia kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea,kampeni,kura,kuhesabu kura na Kutangaza Mshindi.Kumbuka,Kukiwa na Uchaguzi HURU basi utakuwa ni wa HAKI.

Dhana ya uchaguzi HURU sio swala la kuwa na TUME HURU ya UCHAGUZI bali pia inahusika sana na USHIRIKI MKAMILIFU katika MCHAKATO mzima wa uchaguzi katika hatia.Kushiriki katika mchakato kutatoa nafasi ya kuonesha iwapo kuna UHURU na HAKI.Usiposhiriki katika UCHAGUZI kikamilifu huwezi kusema kwamba uchaguzi sio HURU na wa HAKI

Kwa mfano,iwapo vyomba vya umma vitatumika katika kampeni basi vyama vyote vinapaswa kupewa HAKI SAWA.Iwpo FEDHA ZA SERIKALI ZITATUMIKA KATIKA UCHAGUZI BASI VYAMA VYOTE VIPEWE UKOMO SAWA.

Lengo langu ni kuchokoza mjadala tu.JE kwa kuangalia mchakato wa UCHAGUZI WA MWAKA huu mpaka hatua hii JE unafikiri kwamba tunaweza kusema kwamba UCHAGUZI wa MWAKA HUU bado ni HURU na WA HAKI?
 
Back
Top Bottom