UCHAGUZI CHADEMA: Wanaharakati wanaompigania Lissu mitandaoni wengi wao sio wajumbe wengine Wanachama kabisa wa CHADEMA watamsaidiaje?

UCHAGUZI CHADEMA: Wanaharakati wanaompigania Lissu mitandaoni wengi wao sio wajumbe wengine Wanachama kabisa wa CHADEMA watamsaidiaje?

Master Legendary

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
576
Reaction score
876
Ni ukweli mchungu ila ndiyo ukweli sasa tutafanyaje,hao akina Mwabukusi, Maria,Fatma Karume,Nshala,Dk Slaa,Jebra Kambole,Sativa nk siyo wapiga kura wa Uchaguzi wa CHADEMA ni wapiga kelele tu za kiharakati ambao kiuhalisia hawana madhara kwenye Sanduku la Kura,na wengine siyo wanachama kabisa.

LIssu kipindi chake chote kashindwa kuwashawishi hawa wanaharakati wenzake hata wawe wanachama tu wa CHADEMA, hiki pekee ni kigezo cha kuonyesha Lissu ana udhaifu mkubwa katika kujenga Chama hivyo hafai kuwa Mwenyekiti achana na hizo nyingine za Uongo,Uchonganishi,Fitna na Majungu.

Watanzania tubadilike hizi kelele zisizokuwa na Vitendo hazina umuhimu wowote katika Chaguzi,hata Uchaguzi Mkuu kelele ni nyingi ila kupiga kura Aah!Mwishoni tukipigwa tunabadili kelele kuwa za kuibiwa, Sikatai CCM wanaiba ila na sisi hatuko serious kabisa katika suala la kujiandikisha na kujitokeza kupiga kura.

Hebu Fikiria hao kina Kambole,Maria,Nshala nk wangeona CHADEMA ni muhimu si wangekuwa wanachama na wengine leo si wangekuwa wapiga kura?Wangeshindwa kufanya Mabadiliko?Leo Jebra yuko Clouds kumtetea Lissu hata kadi ya CHADEMA hana ataendesha mabadiliko kwa Kelele?Siasa ni Sayansi siyo Miujiza.

Mbowe ni Mwanasiasa anajua Uchaguzi ni Sayansi na Uchaguzi ni Wapiga kura anafanya Mikakati ya kisiasa kisayansi na Kampeni zake kwa wapiga kura.Take it from me narudia Lissu anashindwa asubuhi sana.

Ni mtazamo tu masela msijenge Chuki,Povu Ruksa!
 
Ndio hao hao watakao mshabikia na kumshawishi ajiunge na chama kingine cha siasa baada ya kushindwa vibaya kwa fedheha uchaguzi wa chadema Taifa 🐒
 
ndio hao hao watakao mshabikia na kumshawishi ajiunge na chama kingine cha siasa baada ya kushindwa vibaya kwa fedheha uchaguzi wa chadema Taifa 🐒
Wanao piga kura ni wajumbe kutoka kanda mbali mbali na sio wanachama wote!!
Utafiti wa wajumbe wa kanda zote unaonesha kukubali kuwa Mbowe sasa apumzike awe mzee wa chama ingawa fedha za Samia ndio zi nampa shinikizo kutaka aendelee!
Hata kama Lema nae hamuungi mkono Mbowe hizo kura za ushindi zitatoka kwa Samia?
 
Wanao piga kura ni wajumbe kutoka kanda mbali mbali na sio wanachama wote!!
Utafiti wa wajumbe wa kanda zote unaonesha kukubali kuwa Mbowe sasa apumzike awe mzee wa chama ingawa fedha za Samia ndio zi nampa shinikizo kutaka aendelee!
kwani katiba ya chadema inamkataza? :HAhaa:
 
Back
Top Bottom