Salam Wakuu,
NImekuja Zanzibar (Unguja) kutembea sasa wakati nazurura na kutalii nikakutana na hilo jengo la Uchaguzi House. Nikasema nipate picha ya pale ikiwemo kujikumbusha kuwa nilipita hapo... huwezi kujua wanaweza kubadilisha design ya jengo au likahamishwa sehemu nyingine tukawa na reference kuwa jengo hili lilikuwa linaonekana hivi.
Kwanza picha linaanza ile tunasogea tu dereva tax akasema nawaomba sana hapa msijipie tu picha nendeni ndani kuombe ruhusa, hawaruhusu wenyewe. Nikasema haya ngoja niende ndani kama hawaruhusu waniambie kwanini.
Nikaingia na kupokelewa kwenye mapokezi ya kwanza, nikawaeleza nnachohitaji akasema embu kaa kwanzaπ akauliza eeeh umekuja kufanya nini, nakamjibu nilikuwa na kazi lakini saivi natalii tu nipate na picha ya hili jengo.
Akasema aaah, sasa sisi haturusu! Mjadala ukaanza. Kwanini hamrusu, akaniambia tumeamua tu kufanya hivyo kuwa haturusu, nikamuuliza kwa sababu gani, huwezi tu kuniambia hamruhusu, kuna sheria au tangazo mmeweka na kueleza kwanini? Akaendelea kujibu hivyo ... ndio nakujibu kuwa tumeamua!π«€π«€
Nikamwambia naomba mniruhusu basi niende utawala wanieleze kwanini hawaruhusu tupige picha hiyo front view, maana maelezo yake hayajitoshelezi, hapo akawaka mbogo! Mimi nishakwambia haturusu kwanini ulazimishe?
Kwanza unajua uzito wa hili jengo? Unajua hawa ndio wanampa mamlaka Rais? Kimoyo moyo nkasema maake hapo kwanza ncheke!ππ€£
Washazoea tume inamuweka Rais mpaka wamesahau kama tunapiga kura, nikamwambia hakuna, ila wanasimamia uchaguzi, halafu hii inahusika nini na mimi kupiga picha hiyo sehemu ya mbele?
Akasema sasa nenda, maana naona unaanza kufosi, unalazimisha sana, nikamwambia sio nafosi, sijakubali maelezo yako nataka mtu anaeweza kunipa maelezo ya kurudhisha kwanini nizuiwe kupiga picha, na utaratibu huo umeanza lini wananchi tupate taarifa sahihi, tunawalipa kwa kodi zetu kwanini unikataze kupiga picha?
Akajibu ungekuja kwa shughuli ya kiofisi ungeenda, kama umekuja kutalii nenda makumbusho jamaa alikuwa na kiburi sio poa, nikamwambia na hii ni sehemu yangu ya kutalii, nikirudi zangu bara foto gallery yangu isome pia nilipita hapa.
Akaniambia kwanza lete kitambulisho tutambuane, muda wote huo hakuona umuhimu wa utambulisho wangu sasa anataka kunijua! Unatokea wapi, Dar, Dar sehemu gani..... nipe kitambulisho chako kabisa, nikamuuliza nikikupa kitambulisho utaniruhusu niingie, akajibu hapana kwanza nataka nijiridhishe wewe nani (nikupe kitambulisho mkatume watu kuniteka, naijua hiyooπ
) nikamwambia kumbe ni probality, sasa nikupe kitambulisho cha nini?
Bana yule kaka akaniambia nyanyuka twende nikawa escorted nje, nikamwambia asante bwana ...... kwa ukorofi, kwahiyo nikagonga mwamba hapo, wakagoma hata kunipa mawasiliano ya reception yenyewe!
Sheria House na kwenyewe ni hivyo hivyo, hapa alienda mwanzangu askari pale mlangoni akasema haturuhusu! Ni Kwanini? Mnaficha nini kiasi cha kutukataza kupiga picha front view tu ya jengo?
Nilipata nafasi ya kupita Wizara ya Elimu pia, hapo hata sikupata tabu, mlinzi aliniruhusu fasta tu, nikajiachia na kujichagulia engo - heko kwao.π
Uchaguzi House kwanini hamruhusu tupige picha hapo nje? Ni sheria? Imeanza lini? Na kwa nini nizuiwe kuingia Utawala kupewa tu ufanunuzi? Wananchi hatutakiwi kuhoji? Nyie mnajibu na kuelekeza wananchi wakati tu wa Uchaguzi?π€