SoC04 Uchaguzi huru na haki huanza na mimi kupiga kura. Kura ni sauti yangu

SoC04 Uchaguzi huru na haki huanza na mimi kupiga kura. Kura ni sauti yangu

Tanzania Tuitakayo competition threads

730435

New Member
Joined
Dec 18, 2023
Posts
3
Reaction score
4
Uchaguzi wa Mwaka 2015 Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ilkua 23,161,440 ,waliojitokeza kupiga kura ni 15,596,110 sawa na 67.34%.

Mwaka 2020 idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ilikua 29,754,699 waliojitokeza kupiga kura ni 15,091,950 sawa na 50.72%. Tunaona idadi ya watu wasiopiga kura inaongezeka kwa kasi kubwa na hakuna hatua thabiti zozote zinazochukuliwa kukabiliana na hili.

Sababu ni nyingi zinazopelekea watu kutoshiriki zoezi la upigaji kura .Baadhi ya sababu ni kutokua na imani na tume ya uchaguzi,kuamini kuwa viongozi hawawezi leta mabadiliko yoyote,umbali wa vituo vya kupigia kura,foleni ndefu kwenye vituo siku ya kupiga kura na kukosa elimu sahihi ya faida za upigaji kura.

Madhara yanayoweza jitokeza kwa kutoshiriki upigaji kura ni makubwa sana ukilinganisha na sababu zinazofanya watu wasipige kura.Yafuatayo ni baadhi ya madhara

Kuwa na mashaka na uhalali wa serikali iliokuwepo madarakani.Kama idadi kubwa ya watu hawakupiga kura kuchagua viongozi ina maana kuwa hao waliochaguliwa wamechaguliwa na kundi dogo tuu la watu…Maana halisi ya demokrasia ni nguvu ya watu..kunapokua hakuna ushiriki wa watu katika kupiga kura hii inamaanisha hakuna demokrasia ya kweli na kusababisha watu kukosa imani na sauti juu ya serikali yao.

Kutopiga kura ni kupoteza haki yako ya msingi..Kura ni sauti ya wananchi.Kupiga kura ni sauti ya watu,katika kura ndipo mwananchi anaweza kuelezea ndoto zake,matumaini na matarajio ya Tanzania aitakayo.Haijalishi dini,kabila,mamlaka au pesa kiasi gani kura ya kila mtu ina uzito sawa katika sanduku la kupigia kura na inaweza leta mabadiliko.Kutoshiriki kupiga kura kunapoteza sauti ya wananchi juu ya serikali inayowaongoza.

Kuchelewesha maendeleo.Kwa kutopiga kura unachelewesha maendeleo kwa sababu kuna uwezekano serikali itayopita katika uchaguzi ikawa na sera na mipango mibovu itayopelekea kuchelewa au kutokuwepo na maendeleo kabisa.Muathirika mkubwa wa hili ni mwananchi wa kawaida na si hao viongozi.

Madhara haya yanaepukika endapo kama taifa zima na sio serikali pekee tutachukua hatua..Baadhi ya hatua zinazoweza chukuliwa ni pamoja na

Tume ya uchaguzi iwe huru na ya haki.Endapo uchaguzi utafanyika kwa uhuru na haki itaongeza imani na morali zaidi kwa wananchi kushiriki upigaji kura

Kuongeza uelimishaji sahihi kwa mpiga kura kuhusu umuhimu wa kushiriki uchaguzi.Serikali, vyama vya siasa na taasisi binafsi zinabidi ziongeze nguvu katika elimu ya upigaji kura na sio kusubiri imebaki miezi kadhaa kabla ya uchaguzi ndo waanze kampeni za kushawishi watu kupiga kura.Elimu hii inabidi iwe endelelevu hata baada ya uchaguzi kupita ili iwafikie watu wengi zaidi hii itaongeza idadi ya wapiga kura kwa kiasi kikubwa.

Kuongeza vituo zaidi vya upigaji kura. Umbali wa vituo vya upigaji kura umekuwa kikwazo kwa wengi kushindwa kufika katika vituo hivyo.Vituo viongezwe na viwe karibu na makazi ya watu na rahisi kufikika.

Kupunguza urasimu katika utoaji kadi ya mpiga kura.Kumekua na changamoto katika kanuni na masharti ili uweze kupata kadi ya kupiga kura. Mfano kama sina kabisa kadi siwezi ipata mpaka pale tume itapokuwa inafanya uboreshwaji wa daftari na kiuhalisia pale uboreshwaji ukianza foleni inakua kubwa na watu wanaghairi kujiandikisha.Kanuni nyingine ambayo si rafiki ni hii kadi ikipotea lazima ulipe ili kupata mpya .Lazima tume ikae chini ibadilishe na kuboresha baadhi ya kanuni zao ziendane na hali halisi ili kuvutia watu kupiga kura.

Kuwatengenezea mazingira mazuri watu wa makundi maalum (Walemavu,wazee) kupiga kura. Kuna ulazima wa kuhakikisha watu wote wanapata haki yao ya kura bila kujali hali zao.Kipaumbele kiwekwe zaidi kwa makundi maalum..miundombinu iwe rafiki katika kufika vituoni, elimu juu ya upigaji kura iwafikie wote na hata wagombea wakati wa kampeni wajitahidi kufikia watu wote kwa njia mbalimbali mf kuweka mkalimani wa lugha ya ishara nk.

Kuweka mfumo kuweza kupiga kura mtandaoni.Nchi nyingi zilizoendelea zinatumia mfumo huu kwa mafanikio makubwa. Mtu mwenye vigezo vya kupiga kura akiwa hata yupo nje ya nchi yake, mbali na kituo cha kupigia kura au matatizo ya kiafya anaweza kupiga kura mtandaoni au kwa ujumbe mfupi wa maneno.

Kuandaa vijana wanaokaribia kupiga kura mapema kwa kuwaandikisha miaka 2 kabla ya kutimiza umri wa kupiga kura. Kundi hili liwe kundi la kuangaliwa sana na kupewa elimu na kuwajengea utamaduni wa kujiandikisha na kupiga kura.Uandikishwaji wa awali katika umri wa miaka 16 utakua unawaandaa kimawazo. Tume inakua na taarifa sahihi za vijana hao na hata ufatiliaji unakua rahisi pale watapohitajika kujiandikisha kamili katika daftari la wapiga kura.

Sisi kama nchi wote inabidi tubadili mtazamo wetu na kukataa kupoteza sauti zetu.Sauti hii tunawaongelea hata wale wasioweza kuongea ni kwa ajili yetu na vizazi vyetu. Mgombea mwenye sera zenye tija na kuleta matumaini ya maendeleo tuhakikishe sauti inamchagua na ambae sera zake haziendani na mtazamo na matumaini ya wengi sauti pia imkatae.Tukumbuke sauti yako ni kura yako.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom