Uchaguzi 2020 Uchaguzi huu ni uchaguzi wa matumizi makubwa ya akili kuliko nguvu

Uchaguzi 2020 Uchaguzi huu ni uchaguzi wa matumizi makubwa ya akili kuliko nguvu

waterproof

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2020
Posts
387
Reaction score
349
Mpaka sasa tumejionea jinsi uchaguzi utakavyokua unahitaji akili nyingi, kuanzia kwenye mchakato wa kura za maoni.

Hawa watu wanne ndio wanaotarajiwa kuongoza kampeni za Upinzani 2020. Si watu wa kubeza hata kidogo, karibia wote ni wajuzi wa mambo ya kisiasa, karibia wote wana utimamu mkubwa wa akili, kupambana nao hakuhitaji matamko ya Bashiru Ally Kakurwa na PhD yake wala Swaga za Comrade Polepole. Hawa wanahitaji brain zote za CCM kuunganishwa yaani CCM mpya na Ile ya Zamani kwa pamoja watengeneza team ya kupambana nao.

Hawa watu Wana malengo ya mbali sana, nafuatilia kwa karibu sana movement zao kila mmoja ana potential yake kwa mbali tunaona kama hawajaungana Ila hawa wamebeba agenda ya pamoja. Wote hawa wanajua njia za kupita kimataifa na hapa nchini, yaani hawawezi kupotea njia kirahisi.

Njia sahihi ya ku deal nao ni matumizi makubwa ya akili kuliko nguvu. Hapa ukiwadhibiti kwa nguvu Wana support kubwa Sana ya Beberu hili nalirudia tena na nitalirudia. Nimeangalia approach tunayokwenda nao Hawa watu wanaweza kutuacha mahali.

Huu ni uchaguzi unaohitaji akili za kujustfy Mambo matatu. Moja Uhuru, mbili haki, tatu Demokrasia.

Huu ni uchaguzi ambao vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama havipaswi Kupata hata lepe Moja la usingizi haswa idara yetu nyeti ya Usalama wa Taifa.

Hawa wanapaswa kufuatilia kila kitu kwenye uchaguzi huu, wanapaswa kumfuatilia kila mgombea kwenye uchaguzi huu, wanapaswa kuchambua kila taarifa ya uchaguzi huu. Yaani asilimia 50 plus ya uchaguzi huu idara yetu wanapaswa kulinda Usalama wa nchi na zilizobakia wawaachie wanasiasa na vyama vya Siasa.

Huu sio uchaguzi wa kumwachia Musiba na wanaharakati wengine, huu sio uchaguzi wa kuwaachia wagombea, huu sio uchaguzi wa kuviachia vyama vya Siasa. Huu uchaguzi unahusu Usalama wa nchi.... Ninaamini sifa ya idara yetu ya Usalama lazima uwe vizuri upstairs, hamjawahi kuwaangusha watanzania, Taifa letu linanyemelewa sana, tukikosea tutadhalilika.

Kuna watu wanachukulia kuwa uchaguzi huu ni mrahisi, Mimi kwa maoni yangu nakataa, huu Ni moja ya chaguzi ngumu kabisa kuwahi kutokea nchini. Huu ni uchaguzi wa matumizi makubwa ya akili, kwa pamoja tutalivusha Taifa letu. Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom