ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,553
Ingependeza zaidi ingekuwa mwaka wa uchaguzi inapita kura ya maoni kwa wananchi ili kutoa mawazo na mapendekezo ya ama kufanyike au kutofanyika uchaguzi.
Zoezi la uchaguzi linaendana na gharama kubwa Sana kulifanikisha,ikumbukwe bado tupo katika janga la corona ambalo limetetemesha uchumi wa dunia, kwa nchi masikini kama Tanzania tulitakiwa Sana kuwa makini katika mambo yote ya matumizi
Nije kwenye Mada, hivi mwaka huu kweli kulikua na sababu ya kufanya zoezi la uchaguzi? Kwanini uchaguzi usifanyike 2025 rais atakapotimiza muda wa miaka kumi ?
Pamoja na kua Mimi si mwana ccm lakini bado sioni kwanini tufanye zoezi hilo ambalo matokeo yake(winner) yapo wazi kabisa
Katika siku Chache tu hizi tumesikia baadhi ya viongozi toka chama cha siasa hapa Tanzania Kila mmoja ametangaza kuwania kiti si jambo baya japo palitakiwa kama chama asimamishwe mtu mmoja.... Any way.. Tuache hilo lakini tujiulize hapa hivi ni nani wa kumshinda mh Rais kwenye mpambano huu?
Kwa nia njema kama mtanzania ningeona ingekua vema hizo pesa za uchaguzi huu zingetumbukizwa kwenye afya au miradi mikubwa ambayo bado ipo katika hatua za kati
Mfano kama Ingewezekana kua gharama za uchaguzi ni sawa na kujenga flyover mbili.... Au ni sawa na kuifikisha Sgr morogoro mjini basi kwa mwaka huu ilikua ni bora tuipeleke pesa hii kwenye miradi hiyo mambo yaendelee mbele!
Hayo ni mawazo yangu binafsi nawasilisha.