Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.

Mkuu,
na kata ya Kining'inila imechukuliwa na chama gani?
 
Thread ni kama alerting note kwa CDM against any cookies towards dem winning and securing da constituency. Infact Mwl yule anakubalika sana miongoni mwa kada mbalimbali. ila kwa alichokieleza cjui DED kuibua tuhuma dhidi ya Mwl ili hatimaye awekewe pingamizi its like porojo flani,, anyway its an alert against any mchezo mchafu
 

Hapo kwenye nyekundu pana walakini,unataka kuniambia sehemu hizo ni kama 'egoli' kwa maendeleo kwa kuwa wamekuwa wakifaidi sera nzuri za CCM,ningekuelewa ungeniambia maeneo hayo yamejaa mazuzu CDM wafanye kazi ya ziada kuwazibua ili waanze kufikiri na kutafakari wapigapo kura...
 

Hapo kwenye red! Shule ya Kata hiyo na kuwaza kwako ni ki-Kata Kata vile!! Pole sana. Kama Igunga watu hawajaamka tutawashangaa!
 
mmmhmh!!! ama kweli 'mbaazi zikikosa maua husingizia Jua' chadema mmeshashindwa kabla hata ya mbio kuanza! jimbo lile ni la ccm kwa hiyo litarudi nyumbani kwake! viti tulivyowaazima mnashindwa kuvitunza; bado mnataka vingine? hebu kitunzeni kiti cha shibuda KWANZA ndipo TUTAFIKIRIA kama tunaweza kuwaongeza vingine mwaka 2015; lakini c hiki cha Igunga!
 
<br />
<br />


Huu ni mwisho wa mwisho wa CCM.
Napita tu jamani.
 
Karibu jamvini. Wewe zilete tu hapa jamvini, habari ikifika hapa ujue haipiti bila kufanyiwa kazi, ili mradi iwe ni ya kweli.

Ccm can do anything illegal na kinyume na human right ili tu kutimaza matakwa yao.naamini kabisa kwa asilimia 120% kuwa wamebuni mbinu zote chafu.kama tu chaguzi ndogo za udiwani wanafanya udhalimu ije iwe ubunge?.mathalani uchaguzi wa diwani kata ya susuni wilayani tarime ambalo diwani wake aliuwa usiku akielekea mjini tarmi kwenye ppori la Nyandoto,ccm wakaspeculate kuwa aliyegombe udiwani kwa cdm ambaye ni baba yake na mbunge wa viti maalum Esther Matiko kuwa ndio kanunua watu wamuue kwa madai eti mbunge alimtumia tshs 80ml.

Speculation hizi awali ziligonga mwamba ambapo wanakijiji waligoma kwani wanamjua mzee Nicolas Matiko.Cha ajabu viongozi wa ccm wilaya akiwemo bwana Zakaria ambaye ni katibu mwenezi na mhazina pamoja alikuja hadi dodoma kumconvice mbunge Esther ambaye ni bintiye kuwa amshawishi baba yake asigombee,kwa taarifa nilizonazo mbunge alimwambia kuwa baba yake anautashi wake mwenyewe agombee au asigombee na hiyo ilikuwa ni tarehe 14.8.2011, na mauaji yalitokea 14.7.2011,,cha ajabu baada ya mzee Nicolas kuombwa na wanakijiji agombee na kuridhia kuchukua fomu usiku wa tarehe 15.8.2011 askari wasiopungua 25 wa kanda maalum tarime na rorya walivamia nyumbani kwa mzee huyo usiku wa saa saba na nusu na kumchukua ambapo kesho yake bila kuchelewa walimwandikia mada.

Cha kusikitisha habari iliyopo viongozi wa kata ya susuni, wilaya na mbunge Nyangwine nasikia wanafurahi wakisema sasa kata itarudi kwao kwani threater wao wamweka jela.na inasadikika watamshikilia mpaka ti baada ya uchaguzi kupita kwani mzee huyu na marehemu ndo atleast walikuwa wanaweza shindana.

Nilitaka tu kuonyesha ni jinsi gani mchezo wowote mchafu waweza chezwa na ccm kwa kutumia vyombo vya dola.kwani polisi hao hao walipinga vikali speculatipn za waccm kata.lkn baada maji kuwafika shingoni waajiri wao wamewaamuru kumbabika kesi mzee wa watu.

Na mbaya zaidi nasikia kuna mtuhumiwa mmoja kakamatwa tangu tarehe 17.7.2011 na alikiri kumuua marehemu na anaseme mzee matiko ahusiki lakini mijaa bado imemkomalia mzee wa watu.

CCM goooooooo to the grave........ Ur days r numbered. Wanachadema na wanamapinduzi wote tupinge unyanyasaji na upwokaji huu wa demokrasia.

Kama diwani wa bumera marwa tengera hadi leo walimbambika mada kesi october mwaka jana wakizani watamshinda bado wananchi walimchagua tu.
 

Nenda direct kwamba CUF imeizid CDM nguvu igunga na sio kutoa visingizio ving kujitetea.Mbona mgombea wa CDM alishawahiwekea pingamizi mgombea wa CUF kagera?
 
Kwa jinsi ccm walivyo na mbinu za kimafia sichelewi kuamini
 
huyu DED mbona anatia huruma!! upande mmoja anaogopa kufukuzwa kazi, upande wa pili wananchi wameahidi wataiwinda familia yake kwa mishale kila mwanafamilia kokote watakakokuwa ikiwa atafanya hujuma, wamedai watalenga na kuyaunganisha masaburi kwa mshale, mbona itakuwa balaa, salaaaaaale kama utani vile!!!!! wengine wamefikia hatua ya kusema watamnyang'anya jina lao la kisukuma huyu mhazini wa ccm (Mwigulu madelu ncheemba) naendelea kutafiti watamnyang'anyaje hilo jina, kwani walimpaje,
 
This is purely defensive mechanism na uongo uliokomaa. By da way, nadhani mgombea wa CDM anaogopa kivuli cha historia ya matendo yake. Kwani enzi zake alikula sana hela za wasukuma na wanyantuzu wa Igunga waliokuwa wakiachisha shule mabinti zao kwa lengo la kuwaozesha. Sasa kwa hofu ya kujulikana kwa maovu yake, ndo maana wanaleta hoja za visingizio.
 
Asante kwa taarifa utatupatia habari nyingi mchakato ukianza maana wewe uko jikoni. Asante sana
 
Igurubi ni sekondari ya Kata?
 

Hii inawahusu wana chadema! Halafu wanyantuzu wamehamia Igunga tangu lini?
 
ChiefmTz, kinachofanya useme hoja ni vya visingizio nini? Kwanini usione kuwa defensive mechanism ni ile ya kumuondoa OCD wa Igunga kwenda kummpumzisha Tabora kabla muda wake wa kustaafu?

Tena kafanyiwa hivyo baada ya kupuuza barua iliyotoka CCM ikimtaka adhibiti operation Sangara ya CHADEMA iliyoanza kwa kishindo kikubwa tar 24/7/2011 kwenye kiwanja kilicho mbele ya ofisi ya CCM wilaya? Kwanini usione kuwa ni defensive mechanism kumuhamisha manager wa NMB Igunga Branch kisa eti nichagga kwa hiyo atakampenia CDM, habari hizi sio siri bali ni public knowledge hapa Ig. Kwanini usione kuwa ni defense mechanism kitendo cha DED Magayane kuwa na mahusiano binafsi yasiyo matakatifu na Bi Neema ambae ndie Katibu wa Wilaya wa CCM Igunga? (wala sio siri kamwe, everybody here knows) Kamati ya bunge ya Mrema ilipofanya ukaguzi hapa ilimpata Magayane na hatia ya ufisadi katika ujenzi wa kipande cha lami cha kuelekea Halmashauri, iliamuriwa asimamishwe kazi, kila mtu hapa Igunga anajua hivyo, ghafla wiki iliyopita karejeshwa kwa masharti hayo, hiyo sio defence mechanism ya ruling system?

Ukitaka kujua habari hizi zinavyovuja ni kuwa ndani ya CCM kuna mpasuko mkubwa, a huge conflict of interest, kuna upande unataka kuhakikisha CCM inashindwa Igunga, na sie kina Julian Asange wadogo tunasubiri kuzidaka kama paka anavyosubiri kwenye tundu la kutokea panya.

Hebu imagine CCM ikipoteza jimbo la Igunga, kisha Chenge nae atangaze kujiuzulu ubunge na Lowasa akitabasamu akisubiri zamu! Thubutu! Wataenda kumramba miguu asijiuzulu kuepusha aibu nyingine, lakini CCM ikishinda Igunga, CCM itapata kiburi cha ajabu, magamba yaliobaki yatang'olewa kwa nguvu.

Anyway, taarifa ya vigezo vitakavyotumika kumuengua Mwl Kashindye tumezipeleka kwa makamanda wa CDM, kama tusiporidhika na hatua watakazochukua, basi kuanzia kesho nawaahidi wanajf kuwa nitafungua thread special itakayovitaja waziwazi vipengele vitakavyotumika kumuengua mgombea huyo, tuone kwa uzito wake kama kuna mtu atabisha, wenye kupenda haki wote nina hakika watapanic, bila kujali itikadi za vyama vyao!

Natusubiri hiyo kesho mtaona jinsi "WikiLeaks" ya Igunga inavyofanya kazi, potelea mbali na wakaninyonge, nimeshachoka, najua wanajf wengi watahudhuria mazishi yangu! MGUNGA WA IGUNGA HAUKOSI MIBA!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…