Uchaguzi Kenya ni kaa la moto

Uchaguzi Kenya ni kaa la moto

mkafrend

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2014
Posts
3,047
Reaction score
1,503
Muungano wa upinzani nchini Kenya (NASA) umeendelea kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais yanayotangazwa na tume huru ya uchaguzi nchini humo (IEBC) huku umoja huo ukitaka tume imtangaze kiongozi wao Raila Odinga kuwa mshindi.

Viongozi wa muungano huo wamesema walikutana na wakuu wa Tume ya Uchaguzi na kuwasilisha rasmi malalamiko yao kupitia barua.

Msemaji mkuu wa upinzani, Musalia Mudavadi amabaye aliwahi kuwa naibu waziri mkuu, amesema upinzani umepata maelezo zaidi kwamba matokeo ya uchaguzi yalivurugwa baada ya kudukuliwa kwa mitambo ya IEBC.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, Wafula Chebukati amekanusha taarifa hizo kwa kusema kulikuwa na jaribio la kudukua mitambo hiyo, lakini halikufanikiwa.

Bw Mudavadi amedai mgombea wa upinzani Raila Odinga ndiye aliyeshinda uchaguzi huo mpaka sasa na tayari ameitaka tume kumtangaza Raila Odinga.

“Twamtaka mwenyekiti wa IEBC atangaze matokeo na kumtangaza Odinga na Kalonzo rais mteule na naibu rais mteule wa Kenya mara moja”,amesema Bw Mudavadi kwenye mkutano na Waandishi wa Habari leo.

Kwa mujibu wa sheria nchini Kenya ni kosa mtu yeyote kutangaza matokeo au kusambaza matokeo ambayo hayajatoka katika tume ya taifa ya uchaguzi kwani tume ndio ina mamlaka ya kutangaza matokeo.

My thought:-
Iwapo raila atashikilia msimamo huu anaweza kuleta uvunjifu wa amani - wananchi kupoteza maisha, mali na uchumi kuyumba - waangalizi wa kimataifa walishughulikie kwa haraka na mwafaka upatikane pande zote mbili.
 
Nikawaida yao kupinga matokeo kwa sababu waliwaaminisha wafuasi kuwa watashinda.Matokeo yamekuja otherwise sasa watawaeleza nini wafuasi wao.Kaanani imeshajaa makazi ya walowezi wawaulize wapalestina.
 
Acrobatic is a modern approach everywhere.
Yaan watu wanapenda figisu hatari
 
Huyo anaesema walitaka kudukuliwa alijuaje au walidukuliwa kwanza ndo wakaweka mambo sawa:

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukiwa systems administrator utajua wakati wadukuzi wanahangaika wakijaribu kukudukua. Kuna kitu huwa tunaita DMZ ambayo hupokea mapigo ya wadukuzi ilhali mfumo wako ukiwa salama.
Hata Facebook waliwahi kusema kwamba maelfu ya wadukuzi huhangaika kila siku wakijaribu kupiga mfumo wao.
 
Muungano wa upinzani nchini Kenya (NASA) umeendelea kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais yanayotangazwa na tume huru ya uchaguzi nchini humo (IEBC) huku umoja huo ukitaka tume imtangaze kiongozi wao Raila Odinga kuwa mshindi.

Viongozi wa muungano huo wamesema walikutana na wakuu wa Tume ya Uchaguzi na kuwasilisha rasmi malalamiko yao kupitia barua.

Msemaji mkuu wa upinzani, Musalia Mudavadi amabaye aliwahi kuwa naibu waziri mkuu, amesema upinzani umepata maelezo zaidi kwamba matokeo ya uchaguzi yalivurugwa baada ya kudukuliwa kwa mitambo ya IEBC.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, Wafula Chebukati amekanusha taarifa hizo kwa kusema kulikuwa na jaribio la kudukua mitambo hiyo, lakini halikufanikiwa.

Bw Mudavadi amedai mgombea wa upinzani Raila Odinga ndiye aliyeshinda uchaguzi huo mpaka sasa na tayari ameitaka tume kumtangaza Raila Odinga.

“Twamtaka mwenyekiti wa IEBC atangaze matokeo na kumtangaza Odinga na Kalonzo rais mteule na naibu rais mteule wa Kenya mara moja”,amesema Bw Mudavadi kwenye mkutano na Waandishi wa Habari leo.

Kwa mujibu wa sheria nchini Kenya ni kosa mtu yeyote kutangaza matokeo au kusambaza matokeo ambayo hayajatoka katika tume ya taifa ya uchaguzi kwani tume ndio ina mamlaka ya kutangaza matokeo.

My thought:-
Iwapo raila atashikilia msimamo huu anaweza kuleta uvunjifu wa amani - wananchi kupoteza maisha, mali na uchumi kuyumba - waangalizi wa kimataifa walishughulikie kwa haraka na mwafaka upatikane pande zote mbili.

Uvunjifu wa amani umeletwa na wanaodukua matokeo halali ya wananchi wa Kenya na wala sio Raila!!!
 
pande zinazohusika ziangalie namna bora ya kutatua hili, ila mwisho wa yote I hate politics.
 
Hivi afrika tuna laana gani, nafikiria umefika muda kwa afrika kuangalia njia nyingine ya uongozi ktk nchi zetu ili kuepuka umwagaji damu kama walivyofanya wenzetu waarabu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kwa mtazamo wako Hilary Clinton alipopinga kushindwa na baadhi ya wagombea wa US kutaka kura zihesabiwe upya ilikuwa ni wa Africa?
 
Ndg nisome vizuri, unajua huu mfumo wa vyama vingi tumeufata wa magharibi lkn tukasahau mazingira ya kisiasa nchi za africa na magharibi ni tofauti sana.
Pili ,afrika bado ni wachanga sana ktk mfumo huu ,viongozi wengi ni waloho wa madaraka hawana vipaumbele vya nchi .Jaribu kufikiria jambo dogo kati ya faida na hasara tunazopata baada ya uchaguzi nchi za afrika, anzia burundi, kenya , ivory coast , etc ,ni uharibifu kiasi ilitokea wakati wa uchaguzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi wapinzani wa kenya tunaalani wapinzani wa tz kumuunga mkono uhuru!
 
Back
Top Bottom