Uchaguzi Kenya: Tume ya haki za kibinadamu yasema watu 24 wameuawa

Uchaguzi Kenya: Tume ya haki za kibinadamu yasema watu 24 wameuawa

kilam

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2011
Posts
2,092
Reaction score
2,128
Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya, ambao ulishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, umeapa kuendelea na maandamano wenye nia ya kubatilisha kile ambacho unasema kuwa, matokeo "feki" ya uchaguzi mkuu.

Mpinzani mkuu wa Bw Kenyatta, Bw Raila Odinga, amedai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na wizi mkubwa wa kura.

Seneta James Orengo ameiambia BBC kuwa chama chake, kinachoongozwa na Bw Raila Odinga, hakitapinga matokeo ya uchaguzi mkuu mahakamani, huku akisema kuwa Uhuru Kenyatta tayari ametoa vitisho kwa majaji.

Kufikia sasa watu 11 wameuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu, ambazo zilianza mara tu baada ya Uhuru Kenyatta kushinda kutangazwa mshindi kwa muhula wa pili mnamo usiku wa kuamkia Jumamosi.

Tume ya taifa ya kutetea haki za kibinadamu nchini Kenya, imetoa orodha ya juu ya wahasiriwa wa ghasia hizo huku ikisema kuwa ni watu 24 ndio ambao wameuwawa katika visa vinavyohusiwa na uchaguzi huo, huku ikiongeza kuwa polisi wanatumia nguvu kupita kiasi.

Kaimu Waziri wa usalama wa ndani, Fred Matiangi, amewataja waandamanaji kama "wahalifu".

Kiongozi mmoja mkuu wa chama cha upinzani, Bwana Johnson Muthama, amesema kuwa polisi wanajaribu kuwalazimisha watu "wakubali matokeo hayo."

Uchaguzi Kenya: Tume ya haki za kibinadamu yasema watu 24 wameuawa - BBC Swahili
 
Kumekucha tena Wakenya

sent from Sanduku la Posta using JamiiForums mobile app
 
Kumekucha tena Wakenya

sent from Sanduku la Posta using JamiiForums mobile app
Wapi? Hamna cha kukucha wala nini! Acha wachapwe kiboko tu. Wanasema watu wao wanauliwa wakati ni wao wanawaambia wakavunje maduka ya watu. Hawa jamaa waliingia kwenye mkataba na shetani zamani sana! Wanaomba mauaji yazidi ili nyota yao ya kisiasa iache kufifia!
 
wakora ndio wameuwawa...sio protesters....they tried to take advantage of the situation to steal property...of course there were a few unfortunate cases where the innocent died...
 
Back
Top Bottom