Uchaguzi kenya

Uchaguzi kenya

gmail mkulima

Senior Member
Joined
Jun 11, 2017
Posts
186
Reaction score
114
Nimefuatilia uchaguzi kenya na ningetaka kumshauri raila amollo odinga ajifunze kusoma alama za nyakati, kwanza mh raila aelewe kuna badhi ya makosa makubwa sana aliyafanya tangia siku ya kwanza.
1. Mh raila siku ya kwanza kura zilipoanza kuhesabiwa alikuja na madai kwamba system ya tume imeingiliwa bila kuwa na ushahidi nasema alikurupuka kuja na document ambayo haikuwa na maana hata kidogo hata na utalamu wangu mdogo wa computer nilipoona INTEL 86 nilijua amechemsha sababu hiyo inamaanisha uwezo wa hiyo computer ni 4gb max, je inawezekana tume ikatumia mtambo wa aina hii kuendesha uchaguzi?
2. Dai la Pili la mh raila ni kwamba kura zinazotumwa kutoka majimboni haziendani na zilizopo makao makuu ya tume, kwanza mh raila alikuwa na mawakala ambao walikuwa mashinani na walikubali matokeo na kusaini fomu 34A kisha kutumwa makao makuu ya tume, sasa hapa mahakama ya rufaa ilishatoa uamuzi kwamba kama kutakuwa na tofauti Kati ya matokeo ya jimbo na makao makuu ya tume matokeo ya jimbo ndiyo yatakuwa sahihi.
3 . Wangalizi wote kutoka nje CARTER FOUNDATION E.A.C ,A.U COMESA IGADD wote wameupa uchaguzi a clean bill.
4 kosa kubwa kuliko yote ni kuita kikao na waandishi wa habari na kudai anakura 8m na kenyatta 7m hivyo kuamrisha tume atangazwe mshindi mara moja.
5. Raila ni moja wa viongozi wa afrika ninao wakubali sana kwenye demokrasia lakini kwa hili sikubaliani naye.
6. Hongereni sana wakenya demokrasia ni process malizieni uchaguzi wenu kwa amani mkuze demokrasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom