Elections 2010 Uchaguzi mdogo Igunga: Kipimo tosha kwa vyama hasimu

Wadau niwadokeze tuu mtazamo wangu kama cdm ikishinda igunga kama inavyoelezwa na wadau kuna uwezekano mkubwa wa chama hiki kuchukua dola 2015. Upi mtazamo wenu?

Ni mtazamo finyu sana wa GT km ww, jimbo moja haliwezi ku represent sample ya majibo zaidi ya 290. Na population ya watu igunga ambao ni wapiga kura ambao hawazidi 300,000 haiwezi kuwa sample ya watanzania wapiga kura zaidi ya 15m. Siku nyingine usilete thread km hizi, unatudhalilisha wote humu ndani na kuonekana wajinga kumbe ni sababu ya mtu mmoja tu
 

Hata kumi ilianza na moja.
 
Tatizo hujui kuangalia mambo critically. kwanza CCM ikishindwa Igunga kutakuwa na mgogoro mkubwa sana wa ndani kuhusu maswala ya kujivua gamba. Hasira itawafanya wagombane sana kikao cha NEC kijacho na NEC inaweza kuvunjwa na mgogoro mkubwa sana utaibuka. Hivyo kushindwa CCM si idadi ya kura tu ila mgogogro wa ndani
 
CCM ikishindwa IGUNGA ndo maamuzi ya KiMungu na hawanauwezo wa kurudi tena madarakani 2015. Wantaznia tumekosa mtu wa kututetea dhidi ya udhalimu wa magamba ni Mungu pekee ndiye ataye wamaliza hawa hatawafanyaje Mungu akishasema OUT haitabaidlika kuwa IN tena!

Chamsingi Chadema ambao ndo wanaonekana huenda wakawarithi Magamba wanatakiwa kutulia na kutotenda kinyume na mapenzi ya Mungu.
Chadema lazima waonyeshe si wao wanaopambana na hili joka bali ni Mungu.
 
 

Mkuu kwa hili ulilolisema nakubaliana na wewe kwa asilimia mia mbili. Uchaguzi wa Igunga iwe CCM imeshinda ama imeshindwa lazima kuwe na gogoro tu na siyo kwamba litaibuka tayari kuna gogoro. Hivi unadhani Samwel Sitta, Kaptain Chilligati, Nnape Nauye na wengineo waliopigwa marufuku wasiende Igunga watajisikiaje CCM ikishinda: Simple, nao wameshindwa wao na falsafa yao!!! Kwa upande mwingine wa shillingi haohao watakuwa na hali gani CCM ikishindwa: Watakuwa wameshinda wao na falsafa yao. Hakuna gogoro hapo? Ukiona mnaanza kupigana marufuku na kupeana mipaka ndani ya chombo chenu (Chama) ujue hamkani si shwari tena. Hili gogoro lipo tu ila mungu apishilie mbali lisije kuwagawanya tu hawa CCM na kusambaratika kabla ya uchaguzi wao wa mwakani (2012) na uchaguzi mkuu wa 2015!!
 
Wadau niwadokeze tuu mtazamo wangu kama cdm ikishinda igunga kama inavyoelezwa na wadau kuna uwezekano mkubwa wa chama hiki kuchukua dola 2015. Upi mtazamo wenu?

Nakubaliana na wewe kwa kigezo kimoja tu cha msingi kwamba Igunga ni moja ya ngome za CCM.
Kama ngome za namna hii zikianza kubomoka sasa - miaka 4 kabla ya uchaguzi mkuu - akina Nape watajikuta wako opposition come 2015.
 

kwanini CCM wametumia nguvu nyingi sana
 

kwanini CCM wametumia nguvu nyingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…