fullcup
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 809
- 2,204
Mimi nilikua msimamizi msaidizi wa kituo cha kupigia kura. Mambo yafuatayo niliyoyaona katika kituo yanathibitisha hoja yangu.
1: Kufungua kituo
Kituo kilifunguliwa SAA moja kamili na msimamizi wa kituo, ufunguzi ukishuhudiwa na mawakala wa CCM na CHADEMA. Mabox yalifunguliwa na kuonekana hayana kitu na yalifungwa mbele ya wapiga kura na mawakala.
2: Upigaji kura
Majina yalibandikwa ya wapiga kura katika kituo. Karani alikagua vitambulisho na kumwelekeza mpiga kura kwangu. Mimi nilihakiki picha iliyokwenye Id na mhusoka na kusoma jina ili mawakala wasikie na msimamizi asikie na kuandika namba ya ID. Mawakala walikua ni wakazi wa eneo husika hivyo wapiga kura wote walikubali kuwa ni wakazi halali. Karatasi ziliandaliwa katika kazingira ya wazi na kuwekwa kwenye masanduku husika kwa uwazi.
3: Hesabu za karatasi
Mimi nilikua natik majina ya waliopiga kura na mwisho nilipata hesabu ya watu 221 ya waliopiga kura huku wapiga kura 229 hawakupiga kura katika kituo hicho. Vibutu (vipande vya karatasi za kupigia kura vinavyobaki baada ya kuchana karatasi ya kura) vilitumika bunda 4 zenye karatasi 50 na ile ya tano zilitumika nusu. Hivyo baada ya zoezi lakupiga kura kuisha hesabu za karatasi zilijazwa.
4: Kuhesabu kura
Wakati wa kuhesabu kura msimamizi wa kituo alihesabu kura zote katika box kabla ya kujua hii ya nani na ile ya nani. Hii ilikua kuondoa dhana ya kuwa labda watu waliingia na kura kwenye viatu. Lakini hesabu zilibaki ni 221. Hatà baada ya kuzigawa kutokana na kura zilizopatikana pamoja na zilizoharibika bado hesabu ilibaki ni 221.
NB: Naomba niseme madai yanayotolewa na viongozi wa vyama vya kisiasa sio sahihi na kama yangekuwepo basi mawakala wasingesaini au wao tu wasingepiga kura. Kama kuna sehemu mawakala waliondolewa basi waangalie namna nzuri ya kutatua changamoto hizo lakini sio kutudanganya kuandamana.