Uchaguzi Mkuu wa 2030: Je, bado kuna ambao mtashiriki?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,439
Reaction score
145,410
Kwa miaka mingi sasa kwenye haya majukwaa ya majadiliano [discussion forums] nimekuwa nikisema kwamba bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi, kuiondoa madarakani CCM kupitia chaguzi, haiwezekani.

Kwa njia ambayo si ya kura na si ya kijeshi, kuiondoa CCM madarakani inawezekana. Lakini hapa sipo kujadili hii njia. Hili ni la siku ingine.

Tokea 2005 nimekuwa nikisema kuwa hakuna kabisa haja yoyote ile kwa watu kushiriki kwenye hizo chaguzi za CCM.

Nimekuwa nikipendekeza watu wazisusie hizo chaguzi kwa sababu hazina maana yoyote ile.

Watu wamenipinga kuhusu kususia hizi chaguzi.

Nimeambiwa kwamba huwezi ukamsusia fisi zizi la mbuzi. Nimeambiwa kila aina ya misemo ya kupinga hoja yangu.

Wengi wa ambao hunipinga ni ama bado wana umri mdogo na hawajaanza kufuatilia hizi siasa zetu kwa muda mrefu au ni watu ambao wamekuwa wakizifuatilia kwa muda lakini ambao ni wepesi sana wa kusahau.

Uzuri wangu mimi kwenye haya ni [1] huwa nina kumbukumbu nzuri sana ya mambo na [2] huwa ni mhalisia…..huwa nayatazama mambo kwa uhalisia wake ulivyo na [3] huwa ni mhukumu mzuri sana wa matukio kwa kufuata na kuzingatia tajiriba ya yale yaliyokwishapita.

Hali hiyo huwa hunifanya niweze kuyaona mambo bila kutumia au kushawishiwa na hisia zangu binafsi juu ya hayo mambo.

Kwa mfano, hata kama hisia zangu binafsi zinataka jambo flani ndo liwe, lakini kwa kuangalia jinsi mazingira yalivyo, siwezi nikajidanganya kwamba yatakuwa vile ambavyo nitamanivyo yawe ilhali ninachokiona sivyo vile nipandavyo kiwe.

Sasa basi, tuje sasa kwenye huu uchaguzi wa 2025 ambao Rais Samuya kashinda kwa kishindo cha kipekee kabisa katika historia ya nchi yetu.

97.6% si ya kitoto. Hata enzi za chama kimoja sidhani kama Nyerere aliwahi kukifikia hicho kiwango.

Kwa idadi ya watu waliompigia, milioni 31 nayo si ya kitoto.

Halafu maajabu mengine ni kwamba tume yetu “huru” ya uchaguzi imeweza kuzihesabu kura milioni 32+ ndani ya siku tatu tu 😂.

Hakika wanastahili pongezi.

Sasa tuache masikhara. Wote tulio na akili timamu tunajua yote hayo ni ya uongo.

Samuya hajapata 97.6% ya kura zilizopigwa.

Hakuna watu milioni 32 na kitu waliojitokeza kupiga kura.

Tume haikuzihesabu hizo kura ndani ya siku tatu kwa sababu hazikuwepo.

Hivyo, hitimisho ni kwamba hiyo tume wamejitungia tu hizo takwimu.

Na kwa vile wamezitunga wakiwa na kiwewe, wakasahau hata kutunga takwimu zilizo karibu na uhalisia na wakaja na kituko cha karne ambacho kimekuwa chambo cha dhihaka katika jumuia ya kimataifa.

Kwa nini tume ya uchaguzi imefanya hivyo?

Jibu ni kwa sababu haiko huru. Hao viongozi wake wameteuliwa na Samuya, ambaye ndo mwenyekiti wa CCM, ndo Rais wa nchi, na ndo aliyekuwa mmoja wa wagombea wa urais.

Hao watu aliowateua kwenye hiyo tume, wana uwiwa [beholden] kwake yeye Samuya.

Huo ni mgongano wa kimaslahi ambao uko wazi na dhahiri kabisa kwa yeyote yule kuuona na kuuelewa.

Huu uchaguzi uliopita ni vizuri ukatumika kama mfano wa kwa nini hakuna haja ya kushiriki chaguzi chini ya mazingira yalivyo hivi sasa.

Hivi ni nani kati yenu anaamini kabisa kuwa mgombea wa urais zaidi ya yule wa CCM ndo anaweza kutangazwa mshindi na hii tume?

Kama wameweza kujitungia tu takwimu basi hata itokee mgombea aliyeshinda si wa CCM, wao watamtangaza huyo wa CCM kuwa ndo mshindi.

Hilo tumeweza kuliona hivi majuzi ambapo kiukweli hakukuwepo na uchaguzi lakini tume ya uchaguzi imemtangaza Samuya kuwa ndo mshindi.

Sawa, katangazwa kuwa ndo mshindi lakini wote, pamoja na yeye mwenyewe, tunajua kuwa kakataliwa na Watanzania na hivyo hana uhalali. Alichonacho ni nguvu ya dola tu.

Na mfano mwingine mzuri wa tume huru ni ule uchaguzi uliofanyika Kenya mwaka 2022.

Raila Odinga ndo alikuwa mgombea aliyeungwa mkono na Rais aliyekuwepo madarakani kwa wakati huo.

Na kimsingi, William Ruto ndo alikuwa mgombea wa upinzani.

Lakini kwa vile Kenya wametuzidi mbali sana kidemokrasia, tume yao ya uchaguzi iliyo huru kuliko hii ya kwetu, iliweza kumtangaza Ruto kuwa ndo mshindi wa uchaguzi.

Ingekuwa enzi zile za kabla hii katiba mpya ya Kenya haijaanza kutumika, si ajabu tume ingemtangaza Odinga kuwa ndo mshindi wa uchaguzi.

Nadhani wengi wenu mtakuwa mnakumbuka jinsi vile ambavyo tume ya uchaguzi ya Kenya ilivyomtangaza Mwai Kibaki kuwa ndo mshindi ile mwaka 2007 wakati kiuhalisia alishindwa na Odinga.

Tume huru ya uchaguzi na sheria bora za uchaguzi ni muhimu sana katika kustawisha demokrasia yetu.

Binafsi naamini kabisa kwa sasa hivi, endapo utampambanisha Tundu Lissu dhidi ya Samuya katika uchaguzi ulio wa huru na haki na mwamuzi asiye na upendeleo, Samuya hawezi kupata hata asilimia 10 ya kura.

Lakini hilo kamwe halitowezekan endapo hatuna tume iliyo huru sambamba na sheria zinginezo za uchaguzi kufanyiwa marekebisho.

Kwa yote haya tuliyoyaona wiki iliyopita, nani kati yenu atashiriki kwenye uchaguzi wa 2030 bila kuwepo na mabadiliko yanayohitajika?

Atakayeshiriki huo uchaguzi akiwa na matumaini ya yeye kushinda au mgombea wake kushinda, basi mtu huyo atakuwa mwendawazimu.

Mnakumbuka nilikuwa nawaambia kwamba JWTZ ni taasisi ya hovyo iliyojaa vilaza? Si mmejionea sasa wenyewe?

Basi na kwenye hili la tume huru endeleeni kuniona hamnazo na mwishowe mtanielewa tu.

Pole nyingi ziende kwa vijana wetu mashujaa waliouliwa na mamluki wa Samuya. Hamtosahaulika na Samuya atailipa tu gharama ya mauti yenu.
 
Watakufa kibudu tu one day, miguu yao nitaiuza kama kwio za kuku barabarani.
 
Jambo la kuleta maudhi ni kwamba, hata tusiposhiriki! Bado makarani wao watatupigia kura nyuma ya pazia, na kumpa shetani wao ushindi wa mezani na wa kishindo!

Sasa katika hali ya kustaajabisha na ya kuleta fedheha! Watu hawakujitokeza kwenda kupiga hizo kura zao! Lakini mgombea wao eti ameshinda kwa asilimia 97.66!! Hizi dharau za wazi kabisa kwa watu wenye akili timamu! Binafsi nawapongeza sana SADC kwa kusimama kwenye ukweli.

Mimi tangu 2019 niliapa humu kutoshiriki kwenye haya maigizo yao. Lakini nina uhakika kuanzia mwaka huo nimepigiwa kura na aidha makarani au tume yenyewe! Je, ni wapi nitaidai haki yangu ya kukataa kupigiwa kura kinyume na matakwa yangu?
 
Achana na asilimia mkuu, hizo angeweza kuzipata kwa haki kabisa kutokana na washindani wake, tatizo kubwa na linalothibitisha hawa watu hawana aibu hata tone ni idadi ya watu waliojitokeza kumpigia kura.​
 
Hakukuwa na sababu za kupiga kura kwa mtanzania "huru".

Kama waliweza kutengeneza kura 32M na kuzihesabu kwa siku chache bila kuwa na mtandao, that's unheard of.
 
Achana na asilimia mkuu, hizo angeweza kuzipata kwa haki kabisa kutokana na washindani wake, tatizo kubwa na linalothibitisha hawa watu hawana aibu hata tone ni idadi ya watu waliojitokeza kumpigia kura.​
Wapiga kura milioni 32 kati ya milioni 37 eti walijitokeza siku ya uchaguzi! Idadi kubwa ambayo haijawahi kutokea tangu nchi ilipopata Uhuru!
Halafu kwenye hiyo idadi, mgombea wa ccm akapigiwa kura milioni 31+!!!! Na aliyemfuatia kutoka Chaumma (Salumu Mwalimu) alipata kurs laki 2 pekee!

Cha kujiuliza hao wapiga kura walipiga hizo kura usiku wa manane, au! Maana siku nzima vituo vyote vilikuwa tupu!
 
Huwa najiuliza sana, ni kwanini wanakubali kuchezea pesa za umma kufanya maigizo ya uchaguzi?​
 
Yaani ni wapumbavu hata aibu hawana kabisa walikaa tu waka kadria kwa ahadi ya kuwapa madaraka vyama pandikizi
 
Kwanza CCM itakuwa na Mgombea yupi wakati huo? Tuanzie hapa kwanza
 
Unaubavu huo washenzi tu nyie mnaandamana mitandaoni kila kukicha
Mbwaa wewe, watu tunauchungu wa kupoteza ndugu zetu kwa kupigwa shaba kama swala mbugani, halafu wewe umeshiba pesa za propaganda unakuja unahalisha tu hovyo mbele za watu, mbwaa kabisa wewe.
 
Until sheria na taratibu za uchauzi zinatakapo badilishwa until then nope
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…