Uchaguzi Mkuu wa 2030: Je, bado kuna ambao mtashiriki?

Haja yako ni CCM kuondoka madarakani,kwa nini?..imekukosea nini?..iondoke kiingie chama gani?..siyo lazima kila mtu apige kura,hata huko uliko si wote hupiga,sisi tutapiga
 
Sijasema watu waache tu kushiriki kupiga kura.

Nielewe vizuri, sawa?

Nasema hivi, watu waache kushiriki kupiga kura hadi hapo yatakapofanyika marekebisho ya msingi.

Marekebisho hayo ni yapi?

1. Katiba mpya.

2. Tume huru ya uchaguzi ambayo haina muingiliano wa kimaslahi na mmoja wa wagombea au chama kimojawapo kinachoshiriki kwenye uchaguzi.

3. Marekebisho au mabadiliko ya sheria za uchaguzi, mfano kutokuweza kwenda mahakamani kuhusu matokeo ya urais.

Sasa kigumu hapo kuelewa ni kipi?

Wewe unaona ni sahihi kushiriki kwenye uchaguzi ambao tume ya uchaguzi iliundwa na Samuya, ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais, na ambaye pia ni mgombea urais katika uchaguzi ambao tume aliyoiteua yeye ndo itausimamia na kuuendesha uchaguzi?

Kwa akili yako wewe unaona ni sawa kabisa kushiriki chaguzi chini ya hayo mazingira?
 
Vyama pandikizi vitaachaje?
Vyama pandikizi hata juzi vilishiriki na vimeishia kuwa vituko tu.

Kwa hiyo vyama pandikizi si hoja hapa.

Dah, ila watu mna vichwa vigumu sana aisee.

Yaani bado hamuelewi kabisa umuhimu wa tume huru ya uchaguzi!!
 
Watu wote hawawezi kuacha/kususia kupiga kura! Hata kama wengi tutasusia huo mchakato, bado kuna chawa na wajinga wachache watashiriki kama ilivyotokea tarehe 29 ya juzi!

Na hao wachache wakijitokeza, ndiyo hiyo tume inahalalisha mchakato kwa kutupigia na sisi ambao hatukushiriki. Do you get me?

Kwa hiyo nakubaliana na wewe kupigania Katiba mpya itakayo mpunguzia Rais wa nchi madaraka makubwa! Lakini pia kuwepo na tume huru kweli ya uchaguzi! Na siyo tume ya kiini macho kama hii ya sasa.
 
Wewe una kichwa kigumu tu. Jamanne njema, ✌️.
 

Tulia ndugu yangu hatujui hata kama katiba itakuwepo. Huyu Mama hana miaka miwili hatakuwepo. Nchi inabadilika sana unajuaje kama kwenye katiba mpya uchaguzi utakuwa 2030
 
Tulia ndugu yangu hatujui hata kama katiba itakuwepo. Huyu Mama hana miaka miwili hatakuwepo. Nchi inabadilika sana unajuaje kama kwenye katiba mpya uchaguzi utakuwa 2030
Umesoma na kuelewa nilichokiandika?
 
Hatutashiriki uchaguzi wowote wala maandamano yoyote kama ilivyokuwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…