Elections 2010 Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA: Kujiandaa kuongoza?

Katika Siasa za Tanzania lazima ufanye hivyo na pia itachukua muda kwa ajili CCM kuendesha siasa za kistarabu kuliko kuwa sasa hivi, Hivyo Chadema ni sawa kabisa kujibu na kuwatuhumu CCM na ndio siasa hizo na pia itakuwa vizuri sana kama nao wakiwa wanakura sahani moja na CCM
 
Mwanafalsafa ukitaka nyeti za Mzee Slaa kaa na aidha Cardinal Pengo au Askofu Kilaini wakueleze vizuri,kama wakikubali waombe wakueleze ya Episcopal Council miaka ya 80 na early 90's.................etc.

P.S: Omuhaya ati 'Kitandugao'!!!!

Sema ndugu yangu wasikutishe.

Mimi naona Kitila Mkumbo angefikiriwa kwenye uongozi wa Chadema ana sifa za uongozi ukiondoa mtihani wa kishetani uliomkuta na House Girl wake.

ana uzoefu wa uongozi toka Udsm,msomi hayo na mengine yatawafanya wengi waisikilize Chadema, hata Urais anaweza kusimama.

Mwenyekiti Mbowe aondoke hana sifa za uongozi,background yake haikuwa nzuri huko nyuma,masuala ya kukataa kulipa madeni NSSF,muanzilishi wa Chama kuwa baba mkwe wake inaipa picha Chadema kama ni mali ya mtu au watu fulani au familia fulani,akiondoka yeye na kupewa KITILA MKUMBO itaondoa picha ya uchagga kuwa chama ni cha wachagga.

vyema uchaguzi ukafanyika haraka ili viongozi wapya waweze kujipanga vizuri.

Lwekatare apewe ukatibu mkuu au naibu kwani ana uzoefu wa uongozi amekuwa naibu katibu mkuu kwa miaka zaidi ya kumi na Mwanzilishi wa upinzani Tanzania hilo lisisahaulike.

Mwanakijiji nae ni vyema akarudi nyumbani muda ndio huu akachukua nafasi ndani ya Chadema halafu akagombea jimbo lolote nyota yake inawaka sasa asisubiri achukue PhD kama anavyotaka kufanya Zitto Kabwe.
 
Na wewe je utafanmya nini?? Utafanya nini au ndio kuongea tu na kuandika au vipi??
 
Kumfanya nini nani? Kuongea na kuandika ni mchango mkubwa au unasemaje?
Anza na wewe kwanza kushiriki siasa Active, tunataka vijana wengi waende kuungana na wakina Mnyika na Zitto Kabwe pia
 
Waongoze nchi kwa kigezo kipi? kwa kuwa na ofisi za mikoa vijiweni, kwa kuwa na viongozi wa ngazi ya mkoa wanaoshinda vijiwezeni wanaotegemea mlo wa siku kwa baba na mama zao? kwa kuwa na viongozi wa mkoa wanaosubiri ugali wa shikamoo. it will take a long time for chadema, if not to death!
 
Last edited:
Itakuwa na kazi sana, Ila kwa Watanzania tukiamua kufanya mabadiliko mapema sana
 
Ndugu yangu Augustine Moshi hivi Mzee Slaa unamjua vizuri? Au na wewe umeingia kichwa kichwa kwenye ushabiki wa kutaka Slaa agombee Urais? Si kila king'aacho ni dhahabu!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Bishanga,
Wewe unataka tumjuaje Dr. Slaa? Tunamjuwa kwa yale ayasemayo na aliyoyafanya! Kwani wewe unamjuaje DR. Slaa? Labda utuambie!
Mie leo nikiambiwa nimpendekeze nani awe Rais i wouldn't make a mistake pointing Dr. Slaa! He has done his job! At least!
 
Anafaa sana kuongoza na mtu makini sana katika kuleta maendeleo yake na ni makali sana kwa ufisadi
 
Bwana kura zipo vijijini, chama cha Mapinduzi a.k.a Mafisadi, kina enjoy uimara wake kuanzia katika ngazi za vijiji huko, chadema waanze mikakati ya kukipeleka chama chao na kukiimarisha kuanzia katika ngazi hiyo ya vijiji, kuimarisha chama si kukaa DSM tu nafukuzana na wandishi wa habari, chama kinatakiwa kiwe na mizizi ambayo inaanzia kwa katika maeneo ya chini, muda huu kama chadema wanategemea kupanga safu yao ya uongozi, walenge mikakati yao ya kukiimarisha chama chao vijijini.
 
Tatizo la chadema hawako wazi ktk chaguzi zao za ndani,hapo wananchi wengi wana shaka nako,tofauti na wenzao Cuf.. kuna tatizo kubwa hapo. la pili chadema waache kuwarubuni watu,wakiwemo wagombea wa Cuf,aliekuwa mgombea ubunge mmoja wa Cuf alifuatwa na chadema na wakampa pesa,huyu jamaa kabla aliwahi kuwaambia viongozi wake kuwa Chadema wapo ktk operation kwa ajili ya kuimaliza Cuf,viongozi hawakuskiliza lkn baada ya kuwaambia na kuwapelekea zile pesa wakaamini.. inasemekana hata Lwakatare wakati bado yupo kwenye uongozi alibambwa na watu wa Cuf kwenye hoteli moja kubwa,akiongea na Mbowe,alikuwa yeye na mjumbe mwengine wa Cuf,jina namhifadhi ambaye mpaka leo yupo kiti moto bado,lkn yeye anajitetea kuwa amefata tu alikuwa hajui lolote.. sasa naona ni wakati wa Chadema kubadilika,kama wapo tayari kuchukua nchi,lkn wasifate mtindo wa ccm wa kuhonga watu watakuwa hawaaminiwi....
 
Lakini Chadema wamebadilisha viongozi wa juu mara nyingi zaidi hata kulikuwa na mjadala mkali wakati wa Chacha Wangwe kuwania uongozi kwa hiyo nadhani wanajitahidi japo wanatakiwa kujifunza na kuboresha tu kila chama kina vituko umeona CCM juzi juzi UWT na umoja wa wazazi ulikuwaje
 
chadema haiwezi kuanza kufikiria kuongoza taifa wakati viti vya ubunge hata 10 hawana! ..
wajipange kwanza kuanza kujuulikana vijijini ambapo ndio kuna wapiga kura wengi zaidi.

huwezi kujulikana vijijini kama mjini hujulikani
tarime hakuwezi peleka mabadiliko dar, lakini dar kunaweza kupeleka mabadiliko tarime na vijijini. Mabadiliko yanaanzia mjini

chama ni product kama product nyingine,kujulikana na ubora wake ndio utakiuza chadema...
wanatakiwa wahakikishe wanapata angalau majimbo mawili dar, mwanza na arusha
najua watu wengi mmekazania vijijini lakini ukweli ni kwamba vijijini wanaangalia nini kina tokea mjini na kama mjini kuna mabadiliko basi vijijini kutabadilika, kama mjini hamna mabadiliko basi ni shughuli sana huko vijijini.....
 
Haya maneno ni kweli au unaandika tu mzee wangu??
 

tunatakiwa tuwaelimishe wananchi na kuwaambia kuwa wao ndio wananguvu kuliko vyombo vya dola na ni wao ndio wanaweza kuleta mabadiliko
Idadi ya polisi ni kidogo sana na haiwezi kushindana na wananchi wanaotaka mabadiliko, lakini kama wananchi wenyewe wanaotaka mabadiliko ni watano basi polisi ni wananguvu sana......

ukiwaelimisha wananchi watakupa kura na wataandamana lakini polisi hawawezi kukupa kura
 

duh...mkuu unataka kufananisha ya Tanu kugombea uhuru na Chadema kugombea Urais. Nadhani Tanu ilikuwa na full support ya wananchi na haikuwa na mpinzani. Chadema has to face an adversary who has the majority of support in rural areas, has financial strength and has the will and determination to stay in power. Hivi nadhani Uingereza ilikuwa haina wakati tunagombania Uhuru.
 
Kuna vyama ambavyo watu wanaunda kwa sababu sio kujiimarisha vijijini lakini ni kwamba wananchi wamechoka sana na utawala ambao wanafanya ufisadi kila sehemu, hivyo kuna baadhi Nchi zina sheria ambazo watu wanaweza kuunda chama cha siasa hata kama bado miezi sita ya uchaguzi na kushinda dola, kama una watu au wananchi nyuma yenu
 
Kweli mabadiliko ya Katiba ni muhimu sana,kuwekaweka viraka ni janja tuu.Katiba iundwe upya kwa mazingira ya sasa,hivyo Serikali ihimizwe kuhusu hilo ili iandae mazingira ya mabadiliko hayo ya Katiba.
 
Sasa sisi humo ndani na wanaJf tutaanzisha vuguvugu la ladai ya Kikatiba, Mimi nawambia ndugu zangu hii katiba itakuja lete shida sana baada maana Tanzania haieleweki inafuata siasa gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…