Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF

Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
DODOMA: Leo ni siku ya Mkutano wa Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini(TFF) unaofanyika ktk Ukumbi wa St. Gasper.
  • Katika Uchaguzi huo nafasi zinazogombewa ni Urais wa TFF, Makamu wa Rais wa TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
  • Wagombea wa Urais ni Ally Mayay Tembele, Wallace Karia, Frederic Mwakalebela, Shija Richard, Imani Madega na Emmanuel Kimbe.
  • Nafasi ya Makamu wa Rais inawaniwa na Mulamu Ng'hambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Stephen Mwakibolwa na Robert Selasela.
=====
WAGOMBEA sita wamepitishwa kugombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu katika hatua za awali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, msomi Wakili Revocatus Kuuli alitaja wagombea hao kuwa ni Shija Richard, Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Mwakalebela, Ally Mayai na Emmanuel Kimbe.

“Kikao kimekaa leo na kimepitisha majina ya wagombea kwa hatua ya awali na majina yote yatabandikwa kwenye mbao za matangazo kuanzia kesho ,” alisema Wakili Kuuli.

Awali wagombea kumi walichukua fomu kuwania nafasi ya urais lakini mapema Athuman Nyamlani alijitoa hivyo majina ambayo hayakupitishwa ni Fredrick Masolwa, Jamal Malinzi na John Kijumbe kwa sababu mbalimbali.

Katika nafasi ya Makamu wa rais waliopitishwa ni Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Stephen Mwakibolwa na Robert Selasela huku Geofrey Nyange akielezwa kujitoa.

Katika nafasi ya wagombea wa nafasi ya kamati ya Utendaji Kocha mwenye maneno mengi Jamhuri Kihwelo, Bakari Malima, Abdallah Mussa, kwa kushindwa kuwasilisha cheti cha kuthibitisha elimu ya sekondari kwa mujibu wa kanuni ya 9(2) za uchaguzi.

Wagombea ambao hawakupitishwa kwa kukosa uzoefu kwa mujibu wa kanuni ya 9(3) ni Musa Sima, Salehe Alawi, Thabith Kandoro na Hassan Othuman hajapitishwa kwa kukosa uadilifu kwa mujibu wa kanuni ya 9(7) za uchaguzi wa TFF.

Zoezi la kuchukua fomu lilianza Juni 16, 2017 hadi Juni 20, mwaka huu na jumla ya wagombea 74 walichukua na kurudisha fomu kuomba kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo.

Awali mchujo ulianza Juni 23, kwa mujibu wa kanuni ya 11.1 ya Uchaguzi wa TFF lakini kulitokea kutokuelewana kati ya mwenyekiti wa kamati hiyo Wakili Kuuli na wajumbe wa kamati hiyo hali iliyofanya Kuuli kujiuzulu kabla ya Kamati ya Utendaji ya TFF kukaa na kuivunja kamati hiyo na yeye kurejeshwa tena peke yake.

Shaffih Dauda
 
Iwe Uzi maalum wauchaguz wa Tff Leo

Ila mi hakuna mgombea ninaye mkubali

Only sir leodiger Tenga make the best in TFF during his era

But best wishes for the contenders
Atakaechaguliwa afanye kazi

Maaana kuna mgombea anasapotiwa na wabunge na mawaziri lkn sioni km anaweza Fanya kitu kipya pale tff

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Iwe Uzi maalum wauchaguz wa Tff Leo

Ila mi hakuna mgombea ninaye mkubali

Only sir leodiger Tenga make the best in TFF during his era

But best wishes for the contenders
Atakaechaguliwa afanye kazi

Maaana kuna mgombea anasapotiwa na wabunge na mawaziri lkn sioni km anaweza Fanya kitu kipya pale tff

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
Ni nani huyo mgombea?
 
Back
Top Bottom