Uchaguzi 2020 Uchaguzi mwaka huu 2020 waweza kuwa ACT Wazalendo vs CHADEMA

Andika tu kwa kujifurahisha ila CCM itatawala milele na Magufuli atashinda uchaguzi huu kwa wepesi zaidi kuliko uchaguzi uliopita.
Hahahaha😂😂😂😂😂😂 jipe moyo ila mjue msimu huu mnakula ugali na mboga ni pilipili mtatoka kamasi.
 
mkuu endapo ACT ikajidanganya simama peke yake ndo utakua mwisho wake watapigwa propagana moja chali , ngoja wajidanganye MEMBE anafaa but upepo wake nje ni mdogo sidhani kwa mwaka huu hata akipewa kugombea kwa muunganiko wa vyama kama atamtikisa mgombea wa ccm kwa sasa ajipange siku za uson bado ana nguvu tu
 
Bwashee inamaana kule kinondon, ukonga, etc hyo nguvu ya uma ilikuwa bado haijazaliwa!? Kiufupi tu wapinzn watakaurudi safari hii ni wale vivuli tu kina mbatia
Amini nakwambia siasa za ulaghai mwisho wake ni mwaka huu. Watanzania wamechoka kweli, kilichokuwa kinakosekana ni uwepo wa mtu wa kuwahamasisha wafanye wanalotakiwa kulifanya.

Mwaka huu upinzani wanahitaji huyo mtu tu. Wa kuhamasisha nguvu ya umma katika kupiga kura, kulinda kura, kusimamia kuhesabu kura na kutangaza matokeo. Ni hayo tu
 
Vyombo vya dola vipo imara kuliko wakt mwingine wowote, kwa nchi yetu hii ambayo mbongo akiona gwanda tu anaanza kutetemeka usitegemee hicho kitu kamwe.
 
Chadema huwa inachukua nchi kila mwaka sema sisi wananchi ni waoga sana, hatuipi suport ya kutosha chadema, lets say wapiga kura wote wa chadema tungekua na msimamo mmoja wa kusimamia kura bila kuogopa policcm unadhani hivyo vyombo vya dola vingeweza kushindana na nguvu ya umma?
Upinzani wakishindwa kuchukua nchi ntajuwa kuwa wanatumika na ccm na hapo ndo utakuwa mwanzo na mwisho wangu wakuipigia kura chadema achilia mbali ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…