Uchaguzi wa mwaka huu ni muhimu sana kwa watanzania, lakini pia ni mtego mkubwa sana kwa watanzania. Sababu uchaguzi huu ni kati ya Mafisadi na wapigania uhuru wa wanyonge. Ukifuatilia kampeni za CCM si raisi wala mbunge anayeongea jinsi gani atapambana na ufisadi, ni swala ambalo wamelikubali na kwa upande mwingine Dr. Slaa na Chadema wanasema ni jinsi gani watapambana na ufisadi. Ndugu mtanzania hata kama CCM itatoa ahadi 1000, kama swala la kupinga ufisadi halitapewa kipaumbele hizo ahadi ni kazi bure maisha yataendelea kuwa magumu tu, (Naomba usome kwa undani kilichotokea zimbabwe, utaamini ninachosema). Nimalizie kwa kusema hivi mtego mkubwa uliopo mbele yetu ni kuwa KUICHAGUA CCM IENDELEE KUTAWALA NI KURUHUSU MAFISADI KUENDELEA KUIFISADI NCHI YETU(Tusije lalamika katika hilo, si tumetaka wenyewe) na KURUHUSU CHADEMA KUONGOZA NCHI NI KUSEMA TUMECHOKA NA UFISADI NA TUNATAKA UHURU WA WANYONGE