Uchaguzi serikali ya mitaa: CUF ya Pili???

Uchaguzi serikali ya mitaa: CUF ya Pili???

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Posts
3,154
Reaction score
71
Katika mkutano huo natarajia kulieleza taifa mchakato wote wa makubaliano uliofanyika kati ya CUF na CCM... naomba Watanzania waje kwa wingi kuungana na wanafunzi hao na wabunge wa CUF kutoka Ofisi za Bunge kuelekea Nyerere Square.”

Hamad alisema mpaka sasa wananchi wameanza kuelewa umuhimu wa uamuzi huo kwa kuwa wanaendelea kuwahamasisha na wana matumaini makubwa wananchi wataelewa vizuri makubaliano ya kumtambua Rais Karume.
Siku hiyo ya Jumamosi nitaeleza mchakato mzima wa namna chama chetu kilivyotafuta suluhu ya kufikia muafaka,” alisema Hamad.

Maamuzi yaliyofanywa ni matakatifu kabisa na hakuna chembechembe yoyote ya rushwa ikiwa kama kawaida yetu tunatarajia kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu ujao.”

Hamad alisema wakati CCM wanagombana, CUF wanatafuta amani, akisema kuwa chama hicho kikuu cha upinzani visiwani ndicho mbadala kwa uongozi wa Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Mkanyageni, Mohamed Mnyaa alisema licha ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kuonyesha CUF imeshika nafasi ya pili, wanachama hawana budi kuzidi kushirikiana na chama hicho ili kupata ushindi zaidi mwakani.

CUF imekuwa chama cha pili kiushindi licha ya sheria kupindishwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita kwa hiyo chama mbadala ni CUF kote Tanzania Bara na Visiwani” alisema Mnyaa.
Wiki iliyopita Maalim Seif Shariff Hamad aliwaambia wafuasi wa CUF katika mkutano wa hadhara kuwa wamefikia uamuzi wa kumtambua Rais Karume baada ya kutomtambua tangu mwaka 2005 baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu.
 
Tuwapongeze CUF kwa mafanikio yao lakini watuambia vizuri muafaka na CCM vipi?
 
Ya pili maana yake nini? Mshindi ni mmoja tu. CCM.
Washindi wako wengi kuna first, second, third ....and last. kila nafasi ina umuhimu wake. data ndiyo issue lakini hizi ni kauli za wanasiasa wa CUF
 
Goli hili bado halikufanyi MSHINDI!

CUF hawakusema ni Washindi, bali washindi wa Pili. Maana yake kama kuna multiple choice questions all wewe correct answers but CCM was the best answer, that alone does not mean others were not answers, furthermore, probably all were correct answers but cuf was the second most correct answer.

Lazima wajipongeze CUF. Hujasikia watu wanaenda kupiga kura lakini hata uliyopiga haihesabiwi na unapata kura 0? Katika darasa lenye watoto 280, hata aliyeshika namba 200 ni mshindi, aliyeshindwa ni mmoja tu - yule wa 280. Wengine wote wameshinda, lakini aliyeshinda zaidi ni wa kwanza.

Leka
 
Tuwapongeze CUF kwa mafanikio yao lakini watuambia vizuri muafaka na CCM vipi?


Hongera sana CUF. maslahi ya taifa mbele daima kuliko ulafi wa watawala. Wekeni sasa mambo hadharani
 
ungeenda straight to the point na kusema "kafu" yaishinda chadema katika chaguzi za serikali za mitaa, kulikoni kuzunguka na kusema cuf ya pili
 
ungeenda straight to the point na kusema "kafu" yaishinda chadema katika chaguzi za serikali za mitaa, kulikoni kuzunguka na kusema cuf ya pili

Sio CHADEMA tu bali hata NCCR, TLP na vingine vyote.

Hongera sana CUF. kazeni buti sasa mshike hatamu,
 
Hii tu inaonyesha ufinyu wako wa mawazo. Wanawake wameingia vipi humu?

Amandla........

Hata rais wako MKAPA alilitumia sana neno hilo mbona hukumuuliza.au ulikuwa bado mchanga?

nakwambi hata wewe ACHA WIVU WA KIKE
 
Hata rais wako MKAPA alilitumia sana neno hilo mbona hukumuuliza.au ulikuwa bado mchanga?

nakwambi hata wewe ACHA WIVU WA KIKE

Kwa vile kasema Mkapa ndiyo unaona inahalalisha? Na unajuaje kuwa sikumuuliza?

Unazidi kuthibitisha ufinyu wako wa mawazo!

Amandla.......
 
Back
Top Bottom