LGE2024 Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024: Hakuna kupita bila kupingwa, atakapopatikana mgombea mmoja, atapigiwa kura za ndiyo au hapana

LGE2024 Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024: Hakuna kupita bila kupingwa, atakapopatikana mgombea mmoja, atapigiwa kura za ndiyo au hapana

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wanabodi,

Siku ya jana Steven Mutambi, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya TAMISEMI alikuwa akizungumza kwenye mahojiano pale Crown FM na moja ya kauli ambayo alitoa ni kuwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu, ule utaratibu wa mwaka 2020 kwamba wagombea watapita bila kupingwa umeondolewa.

Soma pia: Licha ya Mapungufu, Sheria Mpya ya Uchaguzi Pia ina Mazuri Yake!, Imerejesha Mamlaka ya Uchaguzi kwa Wananchi, Hakuna Kupita Bila Kupingwa!.

Akizungumzia kuhusu utaratibu, Steve alidokeza kuwa tofauti na mwaka 2020 kwenye Uchaguzi huu, hata kama kutakuwa hakuna wagombea kutoka vyama vingine waliojitokeza kuwania nafasi, huyo mgombea mmoja aliyebaki atatakiwa kupigiwa kura ya ndio au hapana.

"Na niombe sana wananchi wajitokeze kwa sababu katika kanuni zinazoongoza uchaguzi wetu safari hii hakuna kupita bila kupingwa. Itafika hatua vyama vya siasa vitaleta wagombea na atakapopatikana mgombea mmoja bado tutatoa fursa kwa wananchi wetu kumpigia kura ya ndio au hapana."

Wakuu mnaonaje utaratibu huu kutoka kwa TAMISEMI ni mzuri au ndo blah blah za kawaida za CCM?

 
Uchaguzi unaosimamiwa na tamisemi binafsi siwezi kushiriki sababu najua utakuwa ni dhulma kwa kwenda mbele ...hali ikiendelea iv ya hawa wateule wa rais kuendelea kusimamia uchaguzi hata uchaguzi mkuu mwakani sitoshiriki pia.
 
CHADEMA HAWATAKI VIJANA WAJIANDIKISHE, JE WANAWAOGOPA KWENYE UCHAGUZI?

Sauti za Chadema sasa zinapaza malalamiko yasiyo na mashiko, wakidai kwamba Tume ya Uchaguzi (NEC) inaandikisha wanafunzi kwa lengo la kuwaandaa kupigia kura CCM. Ukweli ni kwamba, kila kijana mwenye miaka 18 ana haki ya kikatiba kujiandikisha na kupiga kura.

Hii siyo mbinu ya kisiasa bali ni utekelezaji wa sheria, kwani vijana waliozaliwa mwaka 2006, wakiwemo wa umri wa miaka 17 mwaka huu, watafikisha miaka 18 ifikapo mwakani. Je, Chadema wanataka kuwanyima haki zao kikatiba?

Chadema wanatakiwa kuelewa kuwa kila aliyeandikishwa ameonesha kitambulisho kinachoonesha umri wake halali. Kuibua tuhuma za "kuandikisha watoto" bila kutoa ushahidi wa vitambulisho ni mbinu ya kisiasa ya kutengeneza mazingira ya kujiondoa mapema au kutafuta kisingizio endapo watashindwa tena mwakani. Tumeona mbinu kama hizi mara kadhaa—wakishindwa, hukimbilia kusema "tulibambikiwa."

Nani anaweza kuwazuia vijana wenye ari na shauku ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi? Hili si swali la wafuasi wa CCM bali ni ishara ya hofu ndani ya Chadema, wakijua kuwa kizazi cha sasa kinatambua haki zake na hakitadanganywa kirahisi. Wanapojaribu kupinga ushiriki wa vijana, wanaonesha wazi kuwa hawataki sauti za kizazi kipya zisikike.

Kwa kifupi, malalamiko ya Chadema si hoja ya msingi bali mbinu ya kuwatisha vijana na kuwapotezea imani katika mchakato wa uchaguzi. Uchaguzi si mchezo wa kuigiza bali ni nafasi ya kila raia, awe kijana au mzee, kuamua hatma ya taifa kupitia sanduku la kura.

Kama Chadema wana hofu ya kushindwa, basi wanapaswa kujipanga na kuja na sera bora badala ya kutengeneza visingizio visivyo na msingi.
 
Back
Top Bottom