Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Mwenyekiti Kikundi kazi serikali za Mitaa kilicho chini ya Taasisi Policy Forum Bwana Hebron Mwakagenda (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu pendekezo uchaguzi serikali za mitaa kuunganishwa na uchaguzi Mkuu
Wajumbe wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum, wamependekeza uchaguzi wa serikali za mitaa ufanyike mwakani pamoja na uchaguzi mkuu kama ilivyofanya Kenya na Zimbabwe. Mwenyekiti wa Kikundi hicho ambacho kinawakilisha zaidi ya asasi za kiraia 70, Hebron Mwakagenda, alitoa kauli hiyo katika mkutano uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo, Mwakagenda alisema wanamuunga mkono Rais Jakaya Kikwete kuwa, taifa lipo kwenye mtikisiko kuhusiana wa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya. Alisema wanatambua Tamisemi siyo chombo mahususi cha kuendesha chaguzi nchini hivyo wamependekeza uchaguzi wa serikali za mitaa usimamiwe na kuendeshwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kwa sasa wapate nafasi ya kubadilisha sheria za uchaguzi na kufanya maandalizi mengine ili uchaguzi uwe huru.
Alisema kutokana na umuhimu wa uchaguzi huo wameamua kutoa mchango wao katika mchakato huo. Alisema serikali za mitaa zinalenga kupeleka au kuyasogeza madaraka kwa jamii ili kufanya maamuzi, kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma kulingana na matakwa ya wananchi.
Mchakato wa uchaguzi huu unategemea mchakato wa katiba mpya ambao umepoteza ratiba yake ya awali kwa kuwa ingetakiwa kuzinduliwa Aprili 26, mwaka huu lakini upo njia panda,alisema na kuongeza: Mwakagenda alisema wanapenda kufahamu uchaguzi huo utafanyika lini kwa kuwa kwa kawaida kipindi kama hiki kanuni za uchaguzi huwa zimeshaandaliwa na kutolewa.
Alisema kanuni hizo kazi yake kubwa ni kutoa mwongozo na taratibu wa jinsi serikali za mitaa zitakavyoendeshwa.
Pia alisema kikundi chao kinapenda kujua kama kanuni hizo kama zimeandaliwa, ziliandaliwa na chombo gani na ushiriki wa wadau ulikuwaje. Tumeona kwenye vyombo vya habari mkutano wa vyama vya siasa na Tamisemi uliofanyika Morogoro hivi karibuni ambao uliandaa kanuni za uchaguzi wa serikali ambapo kama wadau toka mashirika yasiyo ya kiserikali hatujashirikishwa, alisema.