Uchaguzi simba: Kwanini Azim Dewji asiwaachie Wambura wanasimba wenyewe?

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
5,139
Reaction score
1,147
Mfadhili wa zamani wa Simba, Azim Dewji amesema alichokieleza kuhusiana na njama za TFF kutaka kumrudisha madarakani, Michael Wambura kimekamilika.

Lakini akasisitiza, kukamilika kwake kumekuwa na uwazi na kuonyesha hakukosea hata kidogo.
"Nani anaweza kupinga tena kwamba Wambura amerudishwa kwa hila kama nilivyoeleza.
"Suala la sheria na upigaji kura linatokea wapi, sheria inaamuliwa kwa vipengele.

"Ndiyo maana nilisema TFF ni kawaida yake kufanya maamuzi ambayo yanaiumiza Simba, hii si mara ya kwanza.

"Wao waliofanya hivyo wanajua kuwa walichofanya si sahihi, lengo ni urafiki na kusaidiana.
"Kwa nini kusaidiana kwa maslahi ya watu binafsi badala ya kufuata sheria na kanuni ambazo ziko wazi.

"Sasa hakuna anayeweza kusema nilikuwa nafanya fitna, nilichozungumza nilikuwa nakijua na watu wanielewe vizuri. Sasa imebaki kidogo tu, TFF kuchagua nani awe Rais wa Simba," alisema Dewji.

Wiki iliyopita, Dewji ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa Simba kufika fainali ya Kombe la Caf mwaka 1993, alisema kuwa lazima kamati ya rufaa ya TFF itamrudisha Wambura kugombea nafasi ya urais Simba baada ya kuwa amekatwa na kamati ya uchaguzi ya Simba.

maoni yangu:Azim Dewji,kassim Dewji na wengine wafunge midomo yao wakati huu kuelekea uchaguzi,wajikite katika kumfanyia kampeni mgombea "wao" badala ya kutumia nguvu nyingi kupita kiasi kuhakikisha mgombea "wao" anapita bila challenge,kama walikua hawamuamini mgombea wao huyo kwanini mmoja wao kati ya Azim Dewji na Kassim Dewji hakuchukua fomu za kugombea urais wa simba,kwanini wanajaribu kutaka kuvuruga mchakato wa uchaguzi kwa kuingilia maamuzi ya vyombo husika viliwekwa kwa mujibu wa katiba ya tff,cuf na fifa??wakumbuke kwamba mwisho wa siku wanachama wa simba ndio wenye maamuzi ya mwisho.
 

Hao akina Dewji wanafaidika sana na mali za simba maduka wamepanga na wahalipi pango jezi wanaleta makontena na hawafanywi kitu.
 
Yangoswe muachie ngoswe.
mimi pia ni ngoswe!

kuna kitu kinanishangaza sana,hawa kina dewji na genge lao lote la wanaojiita wenye fedha kwanini hawaamini kwamba wanachama wanao uwezo wa kupembua pumba na mtama,kwanini wanaamini ni wao tu ndio wenye uwezo huo! maana wamekua wakifanya kila jitihada kuhakikisha mgombea wao anapata mtereko kwenye huu uchaguzi kwa kutokua na mpinzani,baada ya jitihada zao kushindwa leo wanajidai kuwalamba miguu wanachama walewale waliokua hawawaamini na kutaka tume ya uchaguzi ndio ichague rais wa simba,leo wanajidai eti wanachama wa simba ni watu wanaojua kiongozi bora ni yupi! azim dewji mi namchukulia kama kiongozi failure tu,aliichukua timu ya sigara ikamshinda,akaichukua moro united toka kwa meley balhabou ikamshika na kushuka daraja,leo anakuja kutuletea mamluki wake alioshindwa nao huko sigara na moro united ndio waje waiweze simba!
 
Dewji Azim na Kassim wanafaidika sana kupitia Simba. ..kiasi wanataka mgombea ambaye atakuja kulinda maslahi yao....
Wambura kwa sasa ndie mtu sahihi kuiongoza Simba na uzuri wanachama wameshabaini hilo....sasa kina Dewji wanahahakumzuia
 
KIM KARDASH na mpira wapi na wapi......JF bwana raha sana.......
 
Last edited by a moderator:
Acheni hoja za kikaburu.Badala ya kujadili hoja kama yeye alivyoitoa mnamjadili yeye kama mtu.Anasema TFF inaelekea kuwachagulia Simba rais.Pia masuala ya sheria huwa hayaamuriwi kwa kura kama ilivyotokea katika kumrejesha Wambura.Semeni kuhusu hoja hizo na si kuangalia biashara za akina dewji.Kwani Manji ni msukuma mbona hahojiwi anapodai yeye ni mkereketwa wa Yanga?
 
Dewji Azim na Kassim wanafaidika sana kupitia Simba. ..kiasi wanataka mgombea ambaye atakuja kulinda maslahi yao....
Wambura kwa sasa ndie mtu sahihi kuiongoza Simba na uzuri wanachama wameshabaini hilo....sasa kina Dewji wanahahakumzuia
Kwa maana nyingine, Wambura hatakiwi kuwa kiongozi wa Simba make watu wote wenye fedha wanaoweza kuisaidia Simba hawamtaki mfano Hans pope, Azim D, Mo na Magori ambaye ni mtu toka kwao. Je yeye atashikiana na nani ili apate pesa za kuendeshea klabu? Tutuvengere pamoja na Ucapitalist wake alikuwa anamgwaya Hans! Na yeye hamtaki Hans, wote wamuungao watakuwa ama Yanga au beneficiaries wake (Wambura)
 

Well said mkuu, watu wanataka kutudanganya mchana kweupeee! Eti mtu aje hataki ufadhili wa watu anataka makampuni TU. Unafikiri kuupata huo udhamini wa makampuni/taasisi unachukua wiki moja tu? sasa hicho kipindi wakati unafanya mipango ya kutafuta wadhamini utaendeshaje timu? Huyu Ismail Aden Rage aliingia Simba na gia hizi hizi za Wambura lakini alipokuwa anaingia mitini pindi timu inapozidiwa na madeni na inapokabiliwa na mechi kubwa na ngumu hususani za mtani wetu Yanga, nani walijitokeza kulipa posho za wachezaji na benchi la ufundi pamoja na kugharamia kambi ua timu? Eti unataka kuja Simba kulinda mali za klabu, FoS ni wezi wa mali za klabu! Crensius Magori na Zakaria Hans Pope wataiba nini Simba? Tutafakari kwa kina jamani. Huyu mtu anayekwenda kuomba pesa za kula kwa Jamal Malinzi ndo aje kulinda mali za Simba!

Karibuni tubishane kwa HOJA
 
Dewji Azim na Kassim wanafaidika sana kupitia Simba. ..kiasi wanataka mgombea ambaye atakuja kulinda maslahi yao....
Wambura kwa sasa ndie mtu sahihi kuiongoza Simba na uzuri wanachama wameshabaini hilo....sasa kina Dewji wanahahakumzuia

Wewe kama ni Simba UNAPOTEA ila kama ni Yanga uko SAHIHI
 
TFF amejaza wahaya sasa anawapeleka simba.
Simba chagueni wanao jua mpira sio wakuja wanaotaka umaaufu kupitia club yenu.
Wambura hana sifa ni mchofu hawezi kuleta la maana simba .
Alishindwa FAT .
Kuweni macho msiingie mkenge na suti
 
TFF amejaza wahaya sasa anawapeleka simba.
Simba chagueni wanao jua mpira sio wakuja wanaotaka umaaufu kupitia club yenu.
Wambura hana sifa ni mchofu hawezi kuleta la maana simba .
Alishindwa FAT .
Kuweni macho msiingie mkenge na suti

acha kutingishika we,wambura hata humjui unapanua tu mdomo
au kwa kuwa wale ni weupe ndio unaamin wanaipenda simba
 
TFF amejaza wahaya sasa anawapeleka simba.
Simba chagueni wanao jua mpira sio wakuja wanaotaka umaaufu kupitia club yenu.
Wambura hana sifa ni mchofu hawezi kuleta la maana simba .
Alishindwa FAT .
Kuweni macho msiingie mkenge na suti

acha kutingishika we,wambura hata humjui unapanua tu mdomo
 
wameifanyia nini hao watu zaidi ya kuiba pesa za simba, hela za pango, mauzo ya jezi nakadhalika! Simba inahitaji wazalendo, wazalendo maskini ndio waliojenga jengo la simba kwa kidogo walichonacho na sio kutegemea magabachori! Kuna watu wengi wenye nia ya kuwekeza simba ila huo ukoo wa dewji unaweka kauizibe, kasim dewji ndiye aliyeuza basi la simba, kama wanapesa waanzishe timu zao kama bakhresa, mbona bakhresa kaweza? Wao wanang'ang'ania nini simba?
 

Kwanini wambura asianzishe yake? Yeye wakuja tu...simba ina wenyewe na sio wabaguzi
Mijitu imetoka bara basi shida tupu mjini
 

Mwanasimba anayetaka FOS wasiingie Madarakani amewahi changia nn? Magori alihoji kuwa watu wajitokeza wakati wa uchaguzi tu ukipita hata uwanjan hawaingii je wanaichangiaje timu? At least FOS wanaleta changamoto kwny Usajili Mashabiki tunataka burudani siyo maneno ya Wambura na kaka yake Tutuvengere. Yanga wamemng'ang'ania YM sababu ya Usajili tu si vinginevyo. Hajawanyia chochote zaidi ya Usajili, Mbona mpaka Mlimpigia Magoti?
 
zama za mpira ni burudani zishapitwa na wakati, sasa hivi mpira ni burudani na maendeleo, mambo ya kutegemea mtu mmoja mmoja kuendesha timu hayatakiwi! huyo mtu akifa leo? timu itaendeshwaje? simba ni taasisi kubwa inayoweza kujiendesha yenyewe na sio kutegemea vijisent vya baadhi ya watu,inawezekana nyie ndio wale wale ambao bado mnaamini nchi yetu haiwezi kuendelea bila misaada kutoka nje ilhali nchi ina rasimali kibao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…