Uchaguzi TEFA waahirishwa, Saanya kuchezesha Azam Vs Yanga

Chipsi yaipembeni

Senior Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
128
Reaction score
92
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Aloyce Komba, imeitisha majalada ya kamati ya uchaguzi ya TEFA na kamati ya uchaguzi ya DRFA baada ya kupokea malalamiko na rufaa kutoka kwa wagombea.

Kamati ya Uchaguz ya TFF imeyaomba majalada hayo ili ijiridhishe na kuona haki inatendeka kwa wagombea wote na baadae tarehe mpya ya uchaguzi itatolewa.

SAANYA KUCHEZESHA AZAM Vs YANGA

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemteua mwamuzi wa kati Martin Saanya kuchezesha mchezo wa Ngao ya Jamii jumamosi, badala ya mwamuzi Israle Nkongo aliyekua amepangwa awali.

Mwamuzi Israel Nkongo anasumbuliwa na matatizo ya misuli ya paja, ambayo itampelekea kukaa nje ya uwanja kwa takribani siku kumi, hali iliyopeleka TFF kumbadilisha mwamuzi huyo kuelekea kwenye mchezo huo wa jumamosi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…