WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DODOMA HONGERENI SAAAAAAAAANA KWA KUGUNDUA, KUAMUA KUISIMAMI NA KUHIFADHI 'HAKI NA UHURU WA KUCHAGUA' KIONGOZI UMPENDAYE CHINI YA MAZINGIRA MARIDHAWA KIDEMOKRASIA PALE TULIKOSHINDWA KAMA TAIFA!!!!!!!!
UDOM hongereni sasa kwa uamuzi wenu wa KUTAMBUA, KUILINDA NA KUHIFADHI KITU 'HAKI NA UHURU WA KUCHAGU katika uchaguzi wenu unaotazamiwa.
Sisi wengine huku uraiani tuliufeli huo mtihani vibaya mno hadi kule WAHISANI WA NDANI YA NCHI kujiamulia kushusha toka 'mbinguni' aina ya viongozi, sawa tu na AKINA MWAISIGA THOBIAS wa ulimwengu huu, ambao busara zao ziliwajulisha kwamba watatufaa sana katika ngazi mbali mbali za uongozi nchini.
Japo watu mtachukulia jambo dogo hili ninalosema lakini endapo huu ugunduzi wenu mpya hapo Chuo Kikuu Cha Dodoma utaweza kusambaa koooote nchini; mijini na vijijini basi huko tuendako kamwe mtu hatokaa atupachishie KIONGOZI MAMLUKI maana kwa jinsi tutakavyolinda haki zetu hizi chini ya KATIBA MPYA mnamo 2015, wala usipime!!!!!!!!!!!!!!!!
Mkumbuke sisi wengine huku Uswahilini sasa hivi tuko katika halii hati hati muda wooote kitaifa kwa sababu tu hatukutambua haki zetu na uhuru wa kuchagua hivyo wala hatuna cha kulinda hapa wala kuhifadhi maana tulizidiwa ujanja kwa kuamini saaana watu hadi TUKAPANDIKIZIWA VIONGOZI ambao hata siku moja hatukuwafikiria watuongoze eti kwa jeuri tu ya fedha zao. Jaamae, kule mtu kujichagulia akipendacho rohoni ni raha kweli kweli!!!
Hata hivyo pamoja na nyinyi kuwa bize katika hatua hiyo ya kuchaguana, msisahau jambo la msingi zaidi linalowafanyeni leo hii mchaguane - ULINZI WA MASLAHI YA UMMA wakati wote kwa kutegemea sana elimu mlioibahatika sawa sawa na jinsi UDSM, vyuo vya elimu ya juu na vyuo vikuu vya Mikoa ya Iringa, Arusha na Mwanza wamekua wakifanya kila mara panapo haja.
Huku tukiendelea kuwaungeni sana mkono kwa kila hatua mnayojishughulisha nayo katika hili la 'UCHAGUZI HURU NA SAUTI HURU VYUONI', hadi hapa sisi wengine huku JF ni kule tu kuwaombeeni heri, demokrasia zaidi haki, amani na uwazi zaidi zitawale katika kila hatua ya shughuli hiyo muhimu sana.
kijana ambaye kwa jina anaitwa mwaisiga thobiasi na abubakiri bashi wamechafua hali ya uchaguzi udom.
vijana hawa wakiwa wananadi sera katika chuo cha elimu na chuo cha sayansi ya jamii wamezomewa huku wakiambiwa hutupigi kura uchaguzi sio huru.mwasiga ambaye alikua ananadi sera katika eneo la block q alizomewa na waalimu watarajiwa akiambiwa mtoa matamko ya kijinga huyu kijana ni yule aliyetoa tamko la kulani wabunge wa chadema akidai kuwa msemaji wa serekali kumbe sio msemaji wa serekali .pia bashi anatuhumiwa kutumwa na mmoja wa mafisadi nawasilisha kwa wana udom