Uchaguzi Uganda 2021: Wanahabari wasio na vyeti vya kuangazia Uchaguzi wazuiwa Uganda

Uchaguzi Uganda 2021: Wanahabari wasio na vyeti vya kuangazia Uchaguzi wazuiwa Uganda

Mufti kuku The Infinity

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2019
Posts
6,053
Reaction score
10,032
Wanahabari wasiokuwa na idhini ya kuangazia uchaguzi mkuu wa Uganda wamezuiliwa kufanya hivyo.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano usiku na Inspekta Jenerali wa polisi nchini humo, Meja Jenerali Paul Lokech amesema agizo hilo litaanza kutekelezwa kuanzia Desemba 31.

Lokech amesema polisi wote na mashirika ya usalama yatawatambua wanahabari ambao wameidhinishwa na Baraza la Habari la Uganda kuangazia shughuli za kampeni na uchaguzi.

Taarifa yake inajiri saa kadhaa baada ya kukamatwa kwa mabloga kadhaa na wachapishaji wengine wa mtandaoni wanaohusishwa na chama cha upinzani cha National Unity Party ambao walikuwa wakiangazia kuzuiliwa kwa kampeni za Bobi Wine na kukamatwa kwa maafisa wa kampeni zake katika wilaya ya kati ya Kalangala.

Chini ya mwongozo mpya uliobuniwa hivi karibuni na Baraza la Habari, wanahabari wote nchini humo kando na kulipa ada ya uanachama na kutimiza masharti mengine wanatakiwa kuwasilisha nakala za kazi zao na maelezo yao ya kibinafsi.

Wanahabari wa kigeni wanatakiwa kuwasilisha cheti cha uadilifu kutoka shirika la Interpol.

Ombi hata hivyo linaweza kukataliwa kwa misingi ya kutokuwa na maelezo ya kutosha, kutopata idhini ya vyombo vya usalama au kutoruhusiwa kukanyaga ardhi ya Uganda.

Hatua kali za uhakiki zilianzishwa muda mfupi baada ya serikali hivi karibuni kuwafurusha wanahabari watatu wa Canada ambao walikuwa wameidhinishwa na Baraza la Habari kufanya kazi nchini humo.

Wiki mbili kuelekea uchaguzi mkuu unaokabiliwa na ushindani mkali, serikali imekosolewa kwa ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari na watetezi wa hakiza binadamu.

Jenerali Lokech amesema agizo hilo jipya litasaidia vyombo vya usalama kuwalinda waandishi wa habari.
 
Cheti cha uadilifu kutoka interpol. This is Africa asee
 
Back
Top Bottom