Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete alipotoka Nigeria kushuhudia zoezi la upigaji kura, uhesabuji kura na utangazaji matokeo, alisema kuwa angependa siku moja nasi Tanzania tufikie kiwango cha Wanigeria.
Mojawapo ya jambo alilolitamka ni kuwa kura zilikuwa zinahesabiwa eneo la wazi huku wapiga kura wakishuhudia. Kura zikiwa zinaoneshwa kwa wapiga kura na mawakala.
Jambo la ajabu hapa kwetu, Tume ya Uchaguzi ya Mahera, msisitizo umekuwa eti mpiga kura akishapiga kura, aende nyumbani, yaani akimaanisha kuwa asishuhudie zoezi la uhesabuji wa kura. Huu nauita ni upuuzi. Unawalazimisha watu waende nyumbani, wasishuhudie process nzima, unataka kuficha nini?
Mtu mwadilifu, ungependa zoezi liwe la wazi sana ili hata mwenye kulalamika akose sababu, na watu wote au wengi inavyowezekana, wawe mashahuda wako kwa jinsi kila hatua, kila kitu kilivyofanyika kwa haki na kwa uwazi.
Wananchi tukatae amri ya kuondoka vituoni baada ya kupiga kura. Wapiga kura wawe huru kuondoka au kusalia maeneo ya upigaji kura alimradi wawe kwenye umbali ambao hauiingilii uhuru wa mtu kupiga kura au watendaji wa Tume kufanya shughuli zao.
Kwa nini tusiige mambo mazuri kama huo mfumo wa Nigeria wa kuhesabia kura hadharani? Kwa nini tunapenda kuiga mambo ya hovyo lakini tunakuwa na kigugumizi cha kuiga mambo mema na yenye tija?
Kama vyombo vya Serikali na taasisi zake, ikiwemo NEC, hawataki kuiga mambo mazuri, sisi wananchi tuna haki ya kuwalazimisha kwa namna zozote tunazoona ni sahihi.
Hata huko kwenye mataifa yaliyoendelea ambako wananchi wanathaminiwa sana katika maamuzi ya Serikali, siyo kwamba Serikali zilikuwa takatifu toka mwanzo, bali wananchi ndio waliozilazimisha ziwe kwa namna ambayo zipo leo. Hapa kwetu wananchi wanalazimishwa mambo ambayo Serikali inayataka. Hilo tulikatae kwa nguvu zetu zote.
Tunapoyakataa mabaya, huku tukiwa na dhamira njema ya kulifanya Taifa letu liwe imara zaidi, na upendo zaidi na umoja zaidi, lazima tutashinda. Siku zote Mungu husimama na watu wema, lakini hakudondoshei, bali hubariki jitihada zako unapopambania haki na wema.
Sent using Jamii Forums mobile app