Pre GE2025 Uchaguzi wa 2025 utakuwa Mpya sana kwa Siasa za Tanzania, Wagombea Ubunge msitegemee mbeleko ya DOLA ni afadhali uweke mzigo mezani!

Pre GE2025 Uchaguzi wa 2025 utakuwa Mpya sana kwa Siasa za Tanzania, Wagombea Ubunge msitegemee mbeleko ya DOLA ni afadhali uweke mzigo mezani!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Uchaguzi Mkuu wa 2025 utakuwa ni wa aina yake sana na wale wanaotegemea kubebwa wajitathmini Kwa Upya

CCM Kwa mfano inaingia kwenye mchakato wa uchaguzi bila wastaafu Muhimu RIP Mkapa na RIP kadhalika Zanzibar inamkosa Kinara wa Siasa zake Maalim Seif RIP

Huu utakuwa kama uchaguzi wa Kambale ambapo hakunaga wa kumuogopa mwenzake kwenye level ya Ubunge na Udiwani

Wapinzani watashinda Ubunge na Udiwani kwenye Ngome zao huu ni Ukweli mchungu na watalinda Kura zao

Uchaguzi huu utatawaliwa na Wapiga kura wa Kizazi cha 2000, Vijana hawa hata wakipewaga Rushwa bado hufanya kile wanachokiamini vichwani mwao kwani wako connected sana

Narudia Kwa wale wabunge wa shujaa Magufuli akina Dr Kigwa na COVID 19 mkilipwa mafao yenu ya Ubunge nendeni mkaimarishe miradi yenu Msibet kurudi bungeni mtapoteza vyote

Baadae Mlale unono 😀
 
Back
Top Bottom