Uchaguzi wa CHADEMA ngazi ya Taifa Sasa ni dhahiri timu mbili za Heche na Mbowe zaanza kutoshana nguvu moja yasikika toka Arusha nyingine toka Singida

Inavyoonekana Kuna mvurugano ndani ya Chadema. Kiini cha kuwepo kwa mvurugano huu huko Chadema kwa maoni yangu ni kutokana na namna Mwenyekiti wa Chama chao hicho Freeman Mbowe kukosa misimamo inayoeleweka kuhusiana na Siasa za nchi hii kwa sasa. Siyo siri hata kidogo, Mbowe akiwa Kama Kiongozi wa Chama Chao hicho, amekuwa ni mtu ambaye Hana msimamo unaoeleweka hali hii imesababisha mkwamo na kuyumba kwa Wanachama wa chama hicho.

Mbowe amekuwa ni mtu asiyeaminika tena kwa sasa ndani ya Chama Chao hicho, watu wengi kwanza wanamchukulia kama ni Mamluki wa Chama tawala ambaye amejipachika kwenye Vyama vya upinzani kwa 'kazi maalumu ya kuvuruga vyama vya upinzani' ili kukinufaisha chama tawala.

'Engine' ya treni ikiharibika mabehewa yote ya treni nayo huyumba na kusimama!
 
Mimi nadhani ni busara huyu Mzee akatulia na kuwaachia wengine waendeleze
 
Heche awe makini
 
Naona HECHE/LISU/MNYIKA wanataka kugusa pasipo gusika.

Bwana LEMA mbeba maono ya DJ bado yupo lakini,atawararuaaa
 
Kila chaguzi una pande/makundi.
Angalia hata chaguzi za ccm kura za maoni waligopigana ngumi hadi wengine wameng'olewa meno.
Na hapo ni serikali ya mtaa ambayo mshahara ni TZS 10,000/=.
Je kwenye maslahi zaidi?????
Think.
 
Sakata la covid 19 unamtoaje mnyika!
 
Mbowe asome alama za nyakati, aking'ang'ania anaenda kukiua chama Moja kwa Moja. Kwa sasa chama kimepalalaizi
 
Huwezi kushindana na mchagga ukatoboa muulize Erythrocyte na Retired
 
Mkuu Erythrocyte niwayakie chaguzi njema, ingawa dosari ya kuufanya during chaguzi za mitaa na vijiji inaweza kuzungumzika na kutatulika
 
Nani kakuambia mbowe atagombea tena,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…