Uchaguzi wa CHADEMA umefungua njia kwa wanasiasa kutambua nguvu ya vijana, CCM wamebadili gia sasa wanaenda na vijana siyo wazee

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kama wewe ni kijana na unaamini katika kulitumikia taifa kama diwani au Mbunge anza kujiandaa kwenda kugombea. Mfumo umebadilika na fikra zimebadilika. Wapiga kura sasa hivi ni vijana na vyama vimebaini umuhimu wa wagombea vijana

Kipenga kimepulizwa anzenu kujinoa, msiseme hakuna mtaji. Mtaji wa 2025 kutokana na hali ya uchumi ilivyo itakuwa ni wapiga kura na siyo kofia na kanga.

Usitafute fedha bali tafuta uungwaji mkono wa wapiga kura. Nendeni kwenye kata na majimbo taifa linawategemea. Bora kukosa ila ukajaribu.

Wakina Wasira kwa upepo huu hawatasimama majukwaani, vijana itabidi wawe jukwaani wazee wakae kimya wasiwakwaze vijana. Ahadi ya mzee haikubaliki
 
Mimi ni mzee kaugonjwa ka kusinzia kananizingua nawaomba ushauri ili niache kusinzia sinzia
ninapotekeleza majukumu yangu ya kitaifa
 
Ndugu , ccm waligundua mapema sana kuhusu vijana, ndio maana unaona enzi za magu aliwatumia sana. Wakati CDM, ilikua ikiwatumia kama red brigade.

Ccm iliamua kuwaweka kazini vijana, wengi sana wametapakaa nafasi za uongozi majimboni.

La mwisho, nafasi hizi hizi za serikali za mitaa 99 percent ni vijana.

Sasa wewe unaongelea ccm gani?
 
Chadema ina wanachama wengi moyoni ila kwa kuwa fursa zipo upande wa pili tumeamua kuwa machawa
 
Ndugu , ccm waligundua mapema sana kuhusu vijana, ndio maana unaona enzi za magu aliwatumia sana. Wakati CDM, ilikua ikiwatumia kama red brigade. Ccm iliamua kuwaweka kazini vijana, wengi sana wametapakaa nafasi za uongozi majimboni,
La mwisho, nafasi hizi hizi za serikali za mitaa 99 percent ni vijana.
Sasa wewe unaongelea ccm gani?
Nguvu ya ccm sio vijana bali ni mbeleko ya vyombo vya dola. Hao 99% hawako kwa ridhaa ya wananchi bali kwa uchaguzi wa kishenzi.
 
Wanaenda na wazee. Hakiki

Wanasahau damu changa kina Nape, Makamba, Bashe, Makonda n.k
 
Kama wewe ni kijana na unaamini katika kulitumikia taifa kama diwani au Mbunge anza kujiandaa kwenda kugombea. Mfumo umebadilika na fikra zimebadilika. Wapiga kura sasa hivi ni vijana na vyama vimebaini umuhimu wa wagombea vijana

Kipenga kimepulizwa anzenu kujinoa, msiseme hakuna mtaji. Mtaji wa 2025 kutokana na hali ya uchumi ilivyo itakuwa ni wapiga kura na siyo kofia na kanga.

Usitafute fedha bali tafuta uungwaji mkono wa wapiga kura. Nendeni kwenye kata na majimbo taifa linawategemea. Bora kukosa ila ukajaribu.

Wakina Wasira kwa upepo huu hawatasimama majukwaani, vijana itabidi wawe jukwaani wazee wakae kimya wasiwakwaze vijana. Ahadi ya mzee haikubaliki
vijna wepi?
 
Back
Top Bottom