Uchaguzi wa CHADEMA umetufundisha jinsi ya kutekeleza demokrasia kwa vitendo, kazi kwenu tume huru

Uchaguzi wa CHADEMA umetufundisha jinsi ya kutekeleza demokrasia kwa vitendo, kazi kwenu tume huru

OPEN the Door

Senior Member
Joined
Nov 15, 2024
Posts
170
Reaction score
84
Tangu CHADEMA kutangaza mchakato wa kumpata Mwenyekiti, wagombea hawakulala, walitoa ya moyoni.Wengi walituhumu, wengine walitoa maneno ya kashifa ili kuvutia kura upande wao, Wenye Hekima na busara walivumilia.

Mwisho wa siku uchaguzi umemalizika. Nilichojifunza katika uchaguzi huu ni kwamba:

1. Uchaguzi ulikuwa HURU,wazi na haki, TUME HURU YA UCHAGUZI inaweza kijifunza kitu hapo?

2.Baada ya uchaguzi, viongozi wa Chadema wanapaswa kuwa kitu kimoja. Walioshindwa katika nafasi zao wasiwaache walioshinda maana wanapaswa kushirikiana na kupeana mikakati ya kukijenga upya chama.

3. Upande wa Diaspora,wakati ndiyo huu sasa kuwekeza hapa, Wahakikishe sasa wakisaidie CHADEMA Kwa hali na mali ili chama hiki kilete ushindani wa kweli Kwa chama Tawala.

4. Nimejifunza kwamba,Freeman Mowe ni kati ya wanasiasa wenye moyo wa kujitoa hadi kukifikisha chama mahali kilipo.

Hakika ni roll modal katika siasa za kidemokrasia Tanzania.

5. Viongozi wapya nawashauri wawe na umoja,wawashauri vyama vingine wauganishe nguvu ili ushindani uwe kati ya CCM na CHADEMA katika uchaguzi mkuu 2025.

Mlolongo wa kugawanya kura Kwa vyama zaidi ya 19 uepukwe. Mfano kura zilipopigwa kati ya wagombea 2,kura zilitosha.

Soma Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Je,wadau mnaonaje ikiwa vyama vya upinzani vitaungana na Chadema kuunda muungano wa kuichalenge CCM katika uchaguzi wa 2025?

Nawasilisha kwenu wadau wa the great thinkers.
 
Back
Top Bottom