Kenya 2022 Uchaguzi wa Kenya kama familia ya kambale kila mtu ana ndevu

Kenya 2022 Uchaguzi wa Kenya kama familia ya kambale kila mtu ana ndevu

Kenya 2022 General Election

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
305
Reaction score
728
Uhuru wa kila mtu kutoa matokeo ya uchaguzi umedhihirisha aibu na fedheha kwa wapenda Demokrasia na wachambuzi wa masuala ya Siasa barani Afrika na Duniani kote. Tume ya Uchaguzi ndio inapaswa kutoa takwimu ili kuepusha mikanganyiko isiyo na tija.

Upande mwingine mshindi wa Ubunge wa Jimbo la Kimilili Bwana Didmus Barasa amedaiwa kumuua msaidizi wa aliyekuwa mshindani wake katika kinyang'anyiro cha Ubunge wa jimbo hilo. Hii ndio maana ya Familia ya Kambale yaani kila mmoja ana ndevu, hakuna kuheshimu sheria.

Jioni hii kituo cha kuhesabia kura cha Kirinyaga kimevamiwa na wafuasi wa wanasiasa Anne Waigiru na mwenzie Wangui Ngirici. Yanayoendelea ni mfano mbaya ambao unapaswa kuchukuliwa kama somo na nchi nyingine ili kuepusha uhuni kutamalaki katika mawanda ya Demokrasia hapa Afrika.

Mchakato wa Uchaguzi nchini Kenya ni mfano mbaya usiopaswa kuigwa hata punje, ni kama Familia ya Kambale kila mmoja anafanya anavyojisikia.
 
tume huru mkuu! yaliyobaki unajilinda mwenyewe ili mpinzani wako kama analengo baya asikudhuru
 
Hizi ni akili duni za kimaskini.
Bila time huru,yangetokea makubwa kuliko hayo.
Kenya sio Kama Tanzania ujue.
 
..tume ya uchaguzi ya Kenya haina matatizo.

..vyombo vya habari ndio vina matatizo.

..ukiritimba na usiri kama wa tume ya uchaguzi ya Tz unatoa nafasi ya wizi na kupika matokeo.
 
Back
Top Bottom