Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Uchaguzi mkuu wa Kenya unategemea kufanyika tarehe 8 August 2017 kuna dalili tosha kuwa sehemu kubwa ya upigaji kura wa wanahama sehemu walipoandikishiwa kupiga kura kwa sababu za kiusalama kuna baadhi ya makabila fulani wameanza kuhama kutoka sehemu ambapo wagombea wao hawana ushawishi katika eneo hilo, kwa mfano watu wa kutoka mikoa ya Nyanza na Magharibi wameanza kuhama kutoka mikoa ya kati ya Kenya, na watu wanaotoka mikoa ya kati wameanza kuhama kutoka mikoa ya Nyanza na Magharibi. Wimbi la watu kuhama litaleta dosari kwa kura za wagombea kwani mtu haruhusiwe kupiga kura sehemu ambapo hakuandikishiwa.
Mgombea wa NASA Raila Odinga amelalamika kwa wapiga kura wake wengi wanaamua kuondoka Jijini Nairobi. Hata wapiga kura wengi wenye asili ya kisomali wameondoka kwa wingi kutoka Nairobi kuelekea mikoa ya Kaskazini mashariki